- APONGEZA MABORESHO HUDUMA TPA

MAMLAKA Ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA,) imepongezwa kwa jitihada zinazoendelea kufanyika ili kuboresha huduma za Bandari ili kukidhi mahitaji ya Soko la ndani na Nchi jirani

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la TPA katika maonesho ya kimataifa ya Wakulima- Nanenane 2023 yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.

Pamoja na pongezi hizo, Mhe. Majaliwa ameilekeza Menejimenti ya TPA kutekeleza kwa haraka mpango wake wa kuwa na miundombinu ya kuhifadhia bidhaa zinazoharibika haraka [ Cold rooms] ili kuongeza tija katika Sekta za Kilimo hasa cha matunda na mbogamboga, mazao ya Mifugo na Uvuvi.

Akimkaribisha Mhe. Waziri Mkuu kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mbossa, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TPA Bw. Nicodemus Mushi amesema, TPA inathamini sana mchango wa Sekta ya Kilimo katika kiwango cha shehena zinazohudumiwa na TPA ambapo, pembejeo za kilimo zinazokwenda kwa Wakulima na mazao ya kilimo kwenda katika masoko ya kitaifa na kimataifa hutegemea huduma za bandari katika usafirishaji wake.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...