Na Shalua Mpanda-TMC

WALIMU katika Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam wameshauriwa kutumia taasisi za kifedha zenye kujali maslahi yao na kuepuka kukimbilia mikopo yenye riba kubwa maarufu kama "kausha damu".

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Matinyi alipokuwa akizungumza na wakuu wa shule za msingi na Sekondari katika Siku ya Walimu wilayani humu iliyoandaliwa na benki ya NMB.

Matinyi amesema ni wakati sasa kwa taasisi za kifedha kuangalia fursa za kufanya kazi na walimu na pia zitoe huduma zinazoendana na kada hiyo ili kuwaepusha na mikopo mitaani isiyo na tija kwao.

"Walimu wakipata huduma bora katika Benki,hawataenda huko kwenye kausha damu....sekta ya ualimu ni kubwa sana,takwimu zunaonesha ni asilimia 22 tu ya watanzania wanatumia huduma za kibemki...hivyo benki zikitoa huduma bora zitawavutia kundi hili kubwa la walimu kutumia huduma hizo, "amsema Matinyi

Kwa upande wake Meneja Mwandamizi Kitengo cha wateja maalum kutoka benki ya NMB Queen Kinyamagoha amesema lengo la kikao hicho ni kukutana na kundi hili maalum la wateja na kujadili fursa mbalimbali.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam(DUCE) na kimewakutanisha walimu wa shule mbalimbali za Msingi na Sekondari katika wilaya hiyo.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...