Rais wa Kituo cha Uwekezaji na Maendeleo cha Waarabu na Afrika (Arab-African Centre for Investment and Development-CAAID), Dkt. Amine Boutalbi amesema kuwa CAAID inaratibu ushiriki wa wafanyabiashara wa Algeria kwenye maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu Maonesho ya Saba Saba kwa mwaka 2024.

Amesema hayo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman Njalikai yaliyofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers tarehe 26 Oktoba 2023.

Aidha, Dkt. Amine Boutalbi ameahidi kuwa CAAID itashirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Algeria kutaratibu kongamano maalum la wafanyabishara wa Algeria litakalofanyika nchini Tanzania mwaka 2024 kwa lengo la kuimarisha uwekezaji na biashara kati ya wafanyabiashara wa nchi hizi mbili.

Kwa upande wake, Balozi Njalikai ameahidi kuwa atashirikiana na kituo hicho ambacho ni kiungo muhimu kati ya Ubalozi na Sekta Binafsi nchini Algeria.

Mhe. Balozi amehidi pia ofisi yake itashirikiana na mamlaka za Tanzania hususan TPSF, TIC na TANTRADE ili kufanikisha ushiriki wa wafanyabiashara wa Tanzania kwenye makongamano ya uwekezaji na biashara yanayoandaliwa na Kituo cha CAAID mwezi Mei 2024.



Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman Njalikai akimkaribisha ofisini kwake Rais wa Kituo cha Uwekezaji na Maendeleo cha Waarabu na Afrika (Arab-African Centre for Investment and Development-CAAID), Dkt. Amine Boutalbi kwa ajili ya mazungumzo

Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman Njalikai akiwa katika mazungumzo na Rais wa Kituo cha Uwekezaji na Maendeleo cha Waarabu na Afrika (Arab-African Centre for Investment and Development-CAAID), Dkt. Amine Boutalbi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...