Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imepokea magari mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 250 kutoka kwa Shirika la maendeleo la Uingereza la UK-AID kwa ajili ya ufuatiliaji na tathimini ya shughuli za kielemu za Program ya Shule Bora nchini.

Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika leo Novemba 16, 2023 katika Ofisi za TET Jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa WyEST, Dkt. Franklin Rwezimula amepokea magari hayo na kuyakabidhi kwa Naibu Katibu OR -TAMISEMI Dkt. Charles Msonde tayari kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa WyEST Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula amelishukuru Shirika la maendeleo la Uingereza la UK-AID kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha Sekta ya Elimu kwa kutoa magari hayo yatayosaidia utekelezaji wa mradi huo.

“Tunashukuru kwa msaada huu, kwani utaimarisha ufuatiliaji na tathimini katika miradi ya elimu na umekuja wakati muafaka kujua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kubaini changamoto mbalimbali”. Amesema Dkt. Rwezimula.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, OR-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amebainisha kuwa, TAMISEMI kama watendaji katika ngazi za mikoa na Serikali za Mitaa wataendelea kutoa ushirikiano kwa mashirika yanayoendelea kusaidia katika kuboresha masuala mbalimbali ikiwemo elimu nchini.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo wa Ubalozi wa Uingereza hapa nchini, Bi.Kemi Williams ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano walionesha katika kuhakisha magari hayo yananunuliwa ili kwenda kusaidia katika utekelezaji wa Programu ya Shule Bora utakaosaidia maboresho katika Sekta ya elimu nchini kupitia ufuatiliaji na tamthimini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba amesema TET kama watekelezaji wa mradi wa Shule bora kupitia mafunzo tayari, imetoa mafunzo kwa walimu na viongozi mbalimbali wa elimu nchini yakiwemo ya mbinu za ufundishaji na ujifunzaji zinazozingatia ujumuishi wa walimu.

Progamu ya Shule Bora inatakelezwa katika mikoa tisa ya Tanzania Bara ambazo zina halamshauri 67 .












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...