Kampuni ya Kilombero Sugar na
Kampuni tanzu za Illovo Sugar Africa, zimeungana kupitia Kampeni yao ya
Kilimanjaro Expeditions kukabidhi taulo za kike 2400 katika shule ya
Sekondari Mieresini kabla ya kuelekea kwenye kilele cha mlima
Kilimanjaro.
Kampeni hiyo itahusisha wapanda mlima 17 kutoka nchi 8 tofauti zilizopo chini ya ABF Sugar Group ambapo wafanyakazi hao wamechaguliwa kupanda Mlima Kilimanjaro, kilele kirefu zaidi barani Afrika. Msafara huo ni wa kuheshimu urithi wa Mandela na una lengo mahsusi la kuchangisha fedha na uhamasishaji kwa ajili ya kushughulikia hedhi salama na kuhakikisha wasichana wanaenda shule katika mazingira mazuri katika nchi zote ambazo ABF Sugar Group wanatoa huduma.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika shule ya Sekondari Mieresini, Marangu Mkoani Kilimanjaro, Meneja Mawasiliano na Mahusiano na Wadau wa Kilombero Sugar, Bw. Victor Byemelwa, alifafanua kuwa msafara huo unalenga kukusanya fedha kwa ajili ya mpango wa kukabiliana na hedhi salama katika jamii ya watanzania na jamii nyinginezo ambapo huduma zao zinapatikana ili kupaza sauti katika kukabiliana na tatizo hili.
Lengo ni kuonesha utofauti na ushirikishwaji wa wapanda mlima kutoka sehemu mbalimbali katika kundi hili na kuonyesha uzuri wa Tanzania kuwa nchi mwenyeji wa kundi hili na kusisitiza Mlima Kilimanjaro kuwa kivutio cha utalii kwa dhamiri.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa kampuni ya Kilombero Sugar, Bw. Fimbo Butallah, alisema kuwa “Kilombero Sugar, pamoja na kampuni tanzu nyingine za ABF Sugar, leo tunakabidhi taulo za kike 2400 kwa shule ya hii ikiwa ni sehemu ya dhamira yetu ya kibiashara katika kustawisha shule na jamii ambazo tunatoa huduma.
Bw. Butallah aliongeza kuwa anafurahishwa na takriban asilimia 60 ya wanafunzi wa shule hii ni wasichana, huku akisisitiza lengo la kuwaweka wasichana shuleni kwa kupambana na hedhi salama. Alisisitiza mipango ya kuendelea kushughulikia ajenda hii kwa kuchangia shule zingine katika mikoa tofauti katika miezi inayofuata. Akihutubia hadhara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, na mgeni rasmi wa hafla hiyo Mhe. Zephania Stephen Sumaye, alibainisha kuwa Serikali ipo tayari na inaunga mkono kila wakati kwa wadau wote wanaounga mkono ajenda za Serikali, ikiwemo sekta ya elimu. Alisema, 'Leo, natoa shukrani zangu za dhati kwa Kampuni ya Kilombero Sugar kwa kushirikiana na jamii kwa namna ya kipekee.'
Akipokea msaada huo wa taulo za kike 2400 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mieresini Bw. Prosper August Mosha alitoa shukurani za jumla za shule hiyo kwa msaada huo huku akisisitiza kuwa umekuja wakati mwafaka na kutimiza malengo yaliyokusudiwa. Shule inakaribisha mipango kama hii kutoka kwa wadau wengine ili kuhakikisha tunaendelea kuweka mazingira mazuri ya kusomea.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...