Na Anangisye Mwateba-Bungeni Dodoma

Wizara ya Maliasili na Utalii, kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) imetenga fedha kiasi cha Shilingi bilioni 23.18 kwa ajili ya matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilomita 2,381.7 na vivuko 69 katika hifadhi za Taifa.

Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Dunstan Kitandula alipokuwa anajibu swali la Mhe. Esther Edwin Malleko aliyetaka kujua Serikali ina mkakati gani wa kuboresha Miundombinu ya Usafiri na Usafirishaji wa Watalii kwenye maeneo ya Hifadhi.

Aidha Mhe. Kitandula aliongeza kuwa miundombinu ya usafiri na usafirishaji wa watalii itaendelea kuboreshwa kwenye maeneo ya Hifadhi za Taifa hapa nchini, kwa kutumia mikakati ya muda mfupi na ya muda mrefu ili kuhakikisha kwamba miundombinu hiyo inapitika wakati wote wa mwaka. Miundombinu hii ni pamoja na barabara, madaraja na viwanja vya ndege.

Mhe. Kitandula alisema kuwa Serikali ya Ujerumani kupitia benki yake ya KfW imekubali kutoa kiasi cha Euro 500,000 ili kugharamia usanifu na upembuzi yakinifu kwa barabara yenye matumizi makubwa katika Hifadhi ya Taifa Serengeti inayounganisha Golini – Lango la Naabi – Seronera yenye urefu wa kilomita 68.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...