SHILINGI Bilioni 18, zimetolewa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), ili kufanikisha ujenzi Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kampasi ya Songea.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Kanali Ahmed Abbas wakati wa hafla ya makabidhiano ya eneo la ujenzi wa IAA kampasi ya Songea kwa Mkandarasi.
Kanali Abbas amesema, ujenzi wa chuo hicho utasaidia kuongeza idadi ya wasomi, kuamsha biashara ndani ya mkoa, uwekezaji katika sekta binafsi sambamba na kukuza huduma za kijamii mkoani Songea.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Kanali Ahmed Abbas amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa jumla ya shilingi Bilioni 18, kwa ajili kufanikisha ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Kampasi ya Songea.


“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Tsh bilioni 18 kwa ajili ya ujenzi wa kampasi hii. Ruvuma tunaenda kukamilisha ndoto tuliyokuwa nayo ya muda mrefu ya kupata chuo kikubwa, chuo hiki kitasaidia kuongeza idadi ya wasomi, kitaamsha biashara ndani ya mkoa, pia kitasaidia kukuza huduma za kijamii na kuchochea uwekezaji katika sekta binafsi”, amesema Kanali Abbas.

Kanali Abbas ameupongeza Uongozi wa IAA kwa uamuzi wa kizalendo wa kufungua Kampasi mkoani Ruvuma , ambayo itatambulisha mkoa kitaifa na kimataifa na itakuwa chachu ya maendeleo ya elimu na kutoa ajira kwa wananchi.

Naye Mbunge wa Songea Mjini na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Damasi Ndumbaro amesema Serikali imefanya kazi kubwa na itaendelea kuleta maendeleo katika mkoa. Amewataka Wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali katika jitihada za kuleta maendeleo kwa wananchi.
Mkuu wa chuo IAA, Prof.Eliamani Sedoyeka pamoja na kumshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo, amewashukuru pia wananchi wa mkoa wa Ruvuma kwa ushirikiano wao wanaouonesha.

Vile vile, Prof. Sedoyeka amesema IAA itajenga jengo lenye hadhi ya kimataifa, huku akibainisha kuwa lengo la IAA ni kuhakikisha kwamba kampasi ya Songea inakuwa kubwa sana katika ukanda wa kusini mwa Tanzania.

Jengo hili litakuwa na ukubwa wa ghorofa tano, uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 4500; ndani yake likiwa na madarasa, maktaba, kumbi za mikutano, ofisi na maabara za Kompyuta. Litajengwa kwa muda wa miezi 12 na Mkandarasi China Aero Technology chini ya msimamizi mshauri Y&P Architect (T) Ltd





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...