Mkuu wa Chuo cha Furahika Dkt.David Msuya na  Mkuu wa Chuo Uuguzi na Ukunga cha Mchukwi Kibiti Malsel Daniel wakionesha hati  za Makubaliano.
Picha ya pamoja kati ya Chuo cha Furahika na Chuo cha afya cha Mchukwi mara kusaini makubaliano.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mchukwi, Dkt Japhet Guzuye akizungumza  kuhusiana na umuhimu wa kuanzishwa kampansi kutokana na uhitaji wa rasilimali watu katika sekta ya afya.

Mkuu wa Chuo cha Furahika Dkt.David Msuya wakibadilishana hati za Makubaliano na Mkuu wa Chuo Uuguzi na Ukunga cha Mchukwi Kibiti Malsel Daniel.
Mkuu wa Chuo cha Uuguzi Mchukwi, Malsel Daniel akizungumza kuhusiana na kusogeza huduma kwa wananchi kusoma kozi ya Uuguzi na Ukunga katika Kampensi mpya ndani ya Chuo cha Furahika.
Mkuu wa Chuo Cha Ufundi Furahika Dkt. David Msuya akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na makubaliano katika Chuo cha Furahika kuanzishwa Kampasi ya Chuo cha Uuguzi na Ukunga Mchukwi wilayani Kibiti katika Chuo cha Furahika jijini Dar es Salaam.


Chalila Kibuda, Michuzi Tv
UONGOZI wa Chuo Cha Uuguzi Mchukwi kutoka wilayani Kibiti mkoani Pwani, kimefungua tawi jipya katika Chuo cha Ufundi, Furahika ambacho kipo Buruguni Malapa jijini Dar es Salaam kwaajili ya kutoa huduma mafunzo ya uuguzi na ukunga kwa ngazi ya cheti na Diploma.

Mkuu wa Chuo cha Uuguzi Mchukwi, Malsel Daniel, akizungumza baada ya kusaini makubaliano ya kuanzisha tawi hilo katika Chuo Cha Furahika, amesema wamekusudia kusogeza huduma hiyo jijini Dar es Salaam ili kwa wahitaji wapate fursa ya kusoma wakiwa karibu na maeneo yao.

Pia ameongeza kuwa sababu nyingine ambayo imewasukuma kufungua tawi lao hapo ni namna uongozi wa Chuo Cha Furahika ulivyotoa ushirikiano wa karibu tangu mchakato ulivyoanza hadi kufikia kusaini makubaliano hayo ambayo dhahiri yatakuwa na tija stahiki.

“Tofauti na hayo, sababu nyingine ya kufungua tawi ndani ya Chuo Cha Furahika, mradi huu utasaidia kusukuma mbele agenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Watanzania wanapata huduma ya afya popote walipo,” amesema.

Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mchukwi, Dkt Japhet Guzuye amesema maono yaliyosababisha kuanzishwa Chuo Cha Uuguzi, Mchukwi kilichopo wilayani Kibiti, mkoani Pwani, pia yamechochea kufungua tawi katika Chuo Cha Furahika jijini Dar es Salaam, hivyo kwao ni furahika kufikisha huduma hiyo katika eneo hilo.

“Kwakweli kwetu ni furaha kufungua tawi hapa kwani maono tuliyoanza nayo kufungua Chuo Cha Mchukwi, tutayaendeleza hapa ambayo tunaamini yatasaidia kuongeza wahudumu katika sekta ya afya hapa nchini, amesema.

Pia, Dkt David Msuya ambaye ni Mkuu wa Chuo Cha Ufundi Furahika, ambacho kimeingia makubaliano na Chuo Cha Uuguzi Mchukwi,kufungua tawi chuoni hapo kwaajili ya kutoa kozi ya Uuguzi na Ukunga, amesema wana madarasa na vitendea kazi vya kutosha kuhakikisha kozi hizo zinatolewa kwa ubora stahiki kulingana na vigezo ambavyo vimewekwa na Mamlaka.

“Kwa kuwa ndoto yetu imetimia nawaomba wazazi kuwaleta watoto wao hapa kwaajili ya kupata mafunzo ya uuguzi na ukunga, pia waingie katika mtandao wa Chuo cha Mchukwi ili waweze kuomba nafasi ya kujiunga na tawi la hapa na tayari dirisha la usahili limefunguliwa”.

Pia niushukuru uongozi wa Chuo Cha Mchukwi kwa kukamilisha jambo hili ambalo limakuja kutimiza ndoto za vijana wetu, pia niishukuru Serikali yetu chini ya Rais Dkt Samia kwa kuendelea kutuunga mkono katika jitihada hizi za kutoa elimu bure kwa jamii yenye uhitaji,” amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...