Mratibu na Muandaaji wa Mbio za NBC Dodoma Marathon, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), leo imetambulisha rasmi na kuitangaza kampuni ya GSM Group kupitia kampuni yake tanzu ya GSM Beverages kama mdau wake mkubwa wa huduma ya maji na vinywaji baridi katika msimu wa sita wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 27 mwaka huu jijijni Dodoma.
Zaidi kuhusu ushirikiano huo, kampuni ya GSM Group kupitia taasisi yake ya GSM Foundation itashiriki katika ufadhili wa agenda kuu za mbio hizo ambazo ni kuendeleza mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, kupanua ufadhili wa wakunga hadi kufikia wakunga 200 pamoja na kuanzisha mpango mpya wa kufadhili masomo ya wauguzi 100 kwa ajili ya watoto wenye changamoto za usonji (autism) nchini.
Hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano huo imefanyika mapema leo jijini Dar es Salaam, ikihusisha maofisa kutoka pande zote mbili. Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa benki ya NBC, Bw Godwin Semunyu aliiwakilisha benki hiyo kwenye makubaliano hayo huku kampuni ya GSM Group ikiwakilishwa na Bw Rajab Kondo ambanye ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko.
Akifafanua kuhusu ushirikiano huo Bw Semunyu alisema kama ilivyo kwa wadau wengine wengi wa mbio hizo, Kampuni ya GSM Group imeguswa na agenda za msingi za mbio hizo na hivyo kuwa sehemu ya harakati hizo za kijamii ambazo kwa msimu huu zinalenga kukusanya fedha kiasi cha Tsh Milioni 700 zitakazosaidia kufanikisha agenda hizo tatu.
“Udhaminiwa kampuni ya GSM Group kwenye mbio hizi unahusisha usambazaji wa maji na vinywaji baridi kwa washiriki takribani 12,000 tunaowatarajia kwenye msimu wa sita wa mbio hizi.’’ Alisema.
“Zaidi GSM Group wameenda hatua nyingine zaidi ambapo kupitia Taasisi yao ya GSM Foundation wameamua kuwa sehemu ya wafadhili muhimu katika agenda zetu hizi tatu ambazo kimsingi zinagusa uhai wa mama zetu na watoto wakati wa kujifungua huku pia mwaka huu tikiangazia zaidi changamoto ya watoto wenye usonji (autism)’’ aliongeza Semunyu.
Kwa mujibu wa Bw Semunyu, kuelekea msimu wa sita wa mbio hizo zitakazohusisha mbio za KM 5, KM 10, Nusu-Marathon (KM 21) na Marathon Kamili (KM 42), benki hiyo inajivunia mafanikio makubwa ya mbio hizo katika kipindi cha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake ikiwemo kukusanya zaidi ya shilingi Billion 1, ambapo zaidi asilimia 80 ya fedha hizo zimeelekezwa katika mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
“Aidha, tumefanikiwa kuwafikia zaidi ya wanawake takribani 47,000 ambapo zaidi ya wanawake 3,000 kati yao wanapatiwa matibabu, na wanawake 1,800 wameripotiwa kupona kabisa na kurejea kwa familia zao. Zaidi, tumetoa ufadhili kwa wakunga 100 kwa kushirikiana na taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation ili kusaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa uzazi (maternal mortarity). Mwaka huu tunatarajia kupanua wigo huu hadi kufikia wakunga 200.’’ Alitaja.
Kwa upande wake Bw Kondo alisema ushirikiano huo unathibitisha jitihada na azma ya pamoja baina ya taasisi hizo mbili katika kukuza afya ya mama na ustawi wa jumla wa jamii huku akikisitiza umuhimu wa ushirikiano na wadau mbalimbali katika kujenga jamii endelevu.
"GSM Group tunafurahi kuwa mshirika mashuhuri wa benki ya NBC katika kufanikisha kusudi hili lenye nia njema kwa jamii tunayoihudumia. GSM Group tunaamini kwa dhati kuwa juhudi za pamoja ni muhimu katika kukabiliana na changamoto zinazokabili jamii zetu. Kwa kutumia ujuzi na rasilimali mbalimbali, tunaweza kuongeza athari yetu na kupanua wigo wetu. Hivyo tunawakaribisha washiriki wengi zaidi waje NBC Marathon kwa kuwa pia tumejipanga kuhakikisha tunakidhi mahitaji yao ya maji na vinywaji vingine baridi,’’ alisema.
Akizungumzia maandalizi ya mbio hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bi Tatiana Masimba alisema mwitikio wa washiriki kutoka ndani na nje ya nchi ni mkubwa huku usajili wa mbio hizo ukiendelea kupitia tovuti ya www.events.nbc.co.tz huku washikiri wakitakiwa kuchangia kiasi cha TZS 45,000 kwa usajili wa mtu mmoja mmoja au 42,000 kwa usajili wa kikundi chenye idadi ya watu 30 au zaidi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za NBC Dodoma Marathon Bi Tatiana Masimba (wa pili kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko wa Kampuni ya GSM Group Bw Rajab Kondo (wa pili kushoto) wakionesha hati ya makubaliano ya ushirikiano wa taasisi hizo mbili ambapo kampuni ya GSM Group kupitia kampuni yake tanzu ya GSM Beverages itakuwa mdau mkubwa wa huduma ya maji na vinywaji baridi katika msimu wa sita wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 27 mwaka huu jijijni Dodoma. Hafla ya kusaini makubaliano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa benki ya NBC, Bw Godwin Semunyu (kulia) na Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM Beverages Bw Ibrahim Jamal (Kushoto)

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za NBC Dodoma Marathon Bi Tatiana Masimba (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kutambulisha rasmi na kuitangaza kampuni ya GSM Group kupitia kampuni yake tanzu ya GSM Beverages kama mdau wake mkubwa wa huduma ya maji na vinywaji baridi katika msimu wa sita wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 27 mwaka huu jijijni Dodoma. Wengine ni pamoja na Mkuu wa taasisi ya GSM Foundation Bi Faith Gugu (kulia), Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko wa Kampuni ya GSM Group Bw Rajab Kondo (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa benki ya NBC, Bw Godwin Semunyu (katikati) na Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM Beverages Bw Ibrahim Jamal (Kushoto)

Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko wa Kampuni ya GSM Group Bw Rajab Kondo akisaini kuthibitisha ushiriki wake kwenye msimu wa sita wa mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27 mwaka huu jijijni Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa benki ya NBC, Bw Godwin Semunyu akisaini kuthibitisha ushiriki wake kwenye msimu wa sita wa mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27 mwaka huu jijijni Dodoma.

Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM Beverages Bw Ibrahim Jamal (Kushoto) akisaini kuthibitisha ushiriki wake kwenye msimu wa sita wa mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27 mwaka huu jijijni Dodoma.

Maofisa wa benki ya NBC pamoja maofisa wa kampuni ya GSM Group wakijipongeza wakati wa hafla fupi ya kutambulisha rasmi na kuitangaza kampuni ya GSM Group kupitia kampuni yake tanzu ya GSM Beverages kama mdau wake mkubwa wa huduma ya maji na vinywaji baridi katika msimu wa sita wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 27 mwaka huu jijijni Dodoma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...