Na MWANDISHI WETU

CHIFU Buhanga wa Kabila la Wasukuma na Wazinza ambaye pia ni mwanaharakati mzalendo wa masuala ya kijami na kisiasa, amezindua kampeni maalumu ya mitandaoni yenye lengo la kuhuimiza kulindwa kwa amani ya taifa na kumuunga mkono Chifu Hangaya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Chifu Buhanga ambaye jina lake halisi ni Laurance Jumanne, amezindua kampeni hiyo, Dar es Salaam, jana, ambayo itajikita kuhimiza jamii kulinda amani na kuunga mkono utendaji kazi wa serikali chini ya Chhifu Hangaya Rais Dk. Samia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kampeni hiyo, Chifu Buhanga amesemaa kwa kiingereza itafahamika kama 'No retreatr No surrender yenye kaulimbiu inayosema Oktoba tunamtaka mama , Zanzibar tunamtaka Mwinyi'.

Amesema kampeni hiyo itahikihimiza vyombo vya dola kuto kurudi nyuma kudhibiti watu na vikundi vinavyo jaribu kuharibu amani ya taifa.

"Tumeshuhudia baadhi ya watu na vikundi kutoka nndani na nje ya nchi vikijiunga kupitia mitandao ya kijamii vikiwa na dhumuni la kufanya upotoshaji na kutaka kusababisha machafuko na umwagaji damu ili nchi iingie katika machafuko kwa manufaa yao binafsi,"ameeleza Chifu Buhanga.

Alisema kampeni hizo ovu zimekuwa zikifanyika katika mitandao na kupewa msukumo mkubwa, hususan kuchochea na kutukana viongozi jambo ambalo halikubariki.

"Baadhi ya watanzania hawajui kilichonyuma ya ya ajenda hiyo ya vikundi viovu vya wanaharakati wa kisisaa mitandaoni. Wapo wananchi wanaounga mkono kwa kufuata mkumbo pasipo kuelewa madhara makubwa yanayoweza kutokea katika taifa. Tutapinga kwa nguvu kubwa mtandaoni,"amesema.

Alisema inasikitisha vijana wengi wameingia katika mkumbo wa kushambulia viongozi jambo ambalo alisema machifu hawaawezi kukubaliana nalo.

"Watanzania waelewe ni bahati kubwa kuwa na kiongozi kama Chifu Hangaya, Rais Dk. Samia. Mama huyu ni mpambanaji ambaye amedhihirisha utendaji wake kwa kukamilisha miradi mingi ya kimkakati,"amebainisha Chifu huyo.

Alisema Chifu Hangaya, Rais Dk. Samia ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu na vyombo vyote vya ulinzi na usalama, visikubari kurudi nyuma katika mapambano ya kulinda amani dhidi ya kampeni ovu zinazofanywa na watu, vikundi au baadhi ya taasisi za kidini kuvuruga amani iliyopo hasa kipindi hiki taifa linapoelekea katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

"NiTuilinde amani hii kwa uchungu mkubwa iwe kwa jasho, machozi na damu. Pia nawaomba waungane nami katika kuendeleza kampeniyangu kuhakikisha tunawajibu kwa uzito wanaotushambulia mitandaoni,"amedai Chifu Buhanga.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...