Na Mwandishi Wetu,Kibaha
WAHITIMU wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (FDC Kibaha)wameshauriwa
kutumia vyema ujuzi wao kama mtaji wa kujenga maisha, badala ya kutegemea ajira pekee.
Ushauri huo umetolewa na Bw. Elisante Joackim Ngure aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 53 ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (FDC Kibaha),mkoani Pwani.
Aidha ametoa mwito wa Kuunda Vikundi na Kutumia Mikopo ya Serikali huku akiwahimiza wahitimu kushirikiana kuunda vikundi vya uzalishaji mali ili kuweza kunufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri nchini kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
“Fursa ipo hivyo nishauri tengenezeni vikundi, vimesajiliwe, halafu ombeni mikopo ya halmashauri,” amesema kusisitiza mwisho wa safari moja ni mwanzo wa safari nyingine.
Amewakumbusha kutumia elimu yenu na ujuzi walioupata kupambana na changamoto za maisha ikiwemo upungufu wa ajira.
Kuhusu maonesho ya Ubora wa Mafunzo yaliyooneshwa na wahitimu yao amesema mafunzo ya vitendo yanayotolewa chuoni hapo yameonesha vijana hawapaswi kusubiri ajira, badala yake wanapaswa kujiajiri, kuajiriwa, na kuajiri wengine.
Akizungumzia kuhusu changamoto zilizowasilishwa kwenye risala ya wahitimu, Bw. Ngure amesema wadau wa elimu wataanza kushirikiana kusaka rasilimali fedha ili kuimarisha chuo hicho kwa manufaa ya vijana na taifa kwa ujumla.
Aidha Ngare kwa niaba ya wadau wa maendeleo, ameahidi kuendelea kushirikiana na chuo na serikali kuhakikisha vijana wanapata mafunzo bora zaidi.“Tunataka kuona vijana wetu wakipata elimu bora itakayojenga maisha yao na kulijenga Taifa.”
Awali akisoma risala kwa niaba ya wahitimu.Godliver Paskali Kingi
amesema Chuo cha Maendeleo ya Wanachi Kibaha kilianzishwa mwaka 1964 kikijulikana kama (Farmers Training Centre) kikiwa na lengo la kuwasaidia Wananchi kuondokana na umasikini kwa kuwapatia Mafunzo ya Kilimo na Ufugaji.
Kuhusu wahitimu amesema walianza Chuo mwaka 2024 wakiwa jumla ya 145 ikiwa wanaume 96 na wanawake 49. “Wanachuo tunaohitimu hii leo idadi yetu ni 112 ikiwa wanume 79 wanawake 33.”
Pia amesema wamepata mafanikio mbalimbali wakiwa chuoni hapo yakiwemo Chuo kumewawezesha kupata Ufundi na Ujuzi wa kutosha ambao utatusaidia, kujiariwa, kujiajiri na kuajiri.
Aidha wameshuhudia Chuo kikitoa Mafunzo ya watu wenye Mahitaji Maalumu jambo ambalo
limewawezesha kushiriki katika maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Ameongeza Chuo kimetoa mafunzo kwa Wanachuo na kuwawezesha kufaulu mitihani yao ya mwisho. Hivyo, kuendelea na Mafunzo katika ngazi nyingine.
“Chuo kimetufundisha Ujuzi tofauti na fani ambazo tumesomea, kama vile Kilimo cha
mbogamboga pamoja na Stadi mbalimbali za maisha.”
Wakati huo huo wahitimu hao wameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya madarasa, Mabweni na Jengo la Utawala na Ofisi za Wakufunzi.
Kupitia risala hiyo wahitimu hao wamesema chuo kinachangamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa Vifaa vya kufundishiwa, udogo wa chumba cha kufundishia Kompyuta na kompyuta kuwa chache ambazo
hazikidhi mahitaji kwa wanachuo.
“Kwa mfano darasa lina wanafunzi 60 ambao
wanahitaji kusoma kompyuta kwa wakati mmoja, lakini Chuo kina kompyuta 20 pekee
na kupelekea kusoma kwa uwiano usio sawa hivyo kupelekea changamoto kwa
Wanachuo na Mkufunzi.”

Bw. Elisante Joackim Ngure aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 53 ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (FDC Kibaha),mkoani Pwani.

Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (KIBAHA-FDC), Bw. Joseph Nchimbi.akisoma hotuba yake wakati wa mahafali ya 53 tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho.

Mgeni rasmi katika mahafali ya 53 ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (FDC Kibaha),mkoani Pwani,Bw. Elisante Joackim Ngure akikabidhi vyeti.

Sehemu ya wanafunzi wa chuo hicho

Picha ya pamoja

Bw. Elisante Joackim Ngure aliyekuwa mgeni rasmi (kulia) akimlisha keki Mkurugenzi wa Huduma za ELIMU, Bw. Jonas Mtangi wakati wa mahafali ya 53 tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (KIBAHA-FDC), Bw. Joseph Nchimbi (kushoto) akilisha keki Bw. Elisante Joackim Ngure aliyekuwa mgeni rasmi wakati mahafali ya 53 tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA,MICHUZI TV)

Bw. Elisante Joackim Ngure aliyekuwa mgeni rasmi wakati mahafali ya 53 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha akimlisha keki mwakilishi wa wanafunzi.

Meza kuu

Mwakilishi wa wazazi na walezi akitoa neno la shukurani wakati wa mahafali ya 53 ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (FDC Kibaha),mkoani Pwani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...