Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika juhudi za kuimarisha utendaji wa taasisi hiyo, hususan katika maeneo muhimu ya ukusanyaji wa mapato.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 17 Disemba 2025, alipokutana na Kamishna Mkuu wa TRA, Ndg. Yussuf Juma Mwenda, pamoja na baadhi ya watendaji wakuu wa Mamlaka hiyo, waliofika Ikulu, Zanzibar, kwa lengo la kujadili masuala ya ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na utoaji wa huduma.
Amesema mapato ni mhimili mkuu wa Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na kuitaka TRA kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma katika kila eneo lenye fursa ya kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato.
Rais Dkt. Mwinyi ameongeza kuwa hatua hiyo ni muhimu kutokana na ukuaji wa kasi wa shughuli za bandari Zanzibar, akitaja Bandari ya Fumba kuwa miongoni mwa bandari zinazokua kwa kasi kufuatia ongezeko la usafirishaji wa mizigo.
Aidha, amebainisha kuwa Serikali imeweka mikakati maalum kwa bandari za Pemba kwa lengo la kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo, hatua itakayowaletea unafuu wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.
Katika mazungumzo hayo, Rais Dkt. Mwinyi amepongeza hatua inayochukuliwa na TRA ya kuweka Scanner mpya bandarini, akibainisha kuwa hatua hiyo itaongeza mapato ya Serikali na kuimarisha usalama wa nchi.
Akizungumzia dhamira ya TRA ya kufanya majadiliano na wadau, Rais Dkt. Mwinyi amesema hatua hiyo ni ya msingi katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo, hususan katika ukusanyaji wa mapato.
Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa TRA, Ndg. Yussuf Mwenda, ameonesha kufarijika na ushirikiano unaoendelea kupatikana kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hali inayochangia kuimarisha utoaji wa huduma za Mamlaka hiyo kwa ufanisi.
Aidha, Kamishna Mkuu huyo amefahamisha kuwa TRA inaendelea na mpango wa kuweka Scanner katika bandari zote nchini kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi na udhibiti wa mapato ya Serikali.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...