SERIKALI imesema inatambua na kuthamini mchango wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) katika kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma jumuishi za fedha kwa wanawake pamoja na wajasiriamali wadogo na wa kati. 

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Elijah Mwandumbya, alipomwakilisha Waziri wa Fedha katika hafla ya kutangaza matokeo ya uorodheshwaji wa Hatifungani ya Stawi Bond chini ya TCB.

Mwandumbya amesema TCB ni benki yenye historia ya zaidi ya miaka 100 katika kuhudumia Watanzania, na utoaji wa Stawi Bond ni uthibitisho wa dhamira ya benki hiyo kuunga mkono Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha. 

Ameeleza kuwa ukusanyaji wa mtaji wa muda mrefu kupitia Stawi Bond utaongeza uwezo wa benki kutoa mikopo nafuu kwa wajasiriamali wadogo, wanawake na vijana, hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi na ajira.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TCB, Adam Mihayo, amesema mafanikio ya kukusanya zaidi ya Shilingi bilioni 140.24 ni ishara ya imani kubwa ya Watanzania kwa benki hiyo na bidhaa zake za kifedha. 

Ameeleza kuwa tofauti na hatifungani nyingi, Stawi Bond imevutia kwa kiwango kikubwa wawekezaji wa kati na wadogo, jambo linaloonesha kuimarika kwa ujumuishi wa kifedha nchini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama, amesema mafanikio ya Stawi Bond yanaonesha ukuaji na mageuzi makubwa katika masoko ya mitaji nchini. 

Amebainisha kuwa hatua hiyo itaongeza ukwasi wa TCB, kuboresha huduma zake na kufungua fursa kwa taasisi nyingine za umma na binafsi kutumia masoko ya mitaji kutafuta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.







Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...