Wananchi wa Kitongoji ya Ormekeke Kijiji cha Nasipaoriong tarafa ya Ngorongoro wameanza kunufaika na mradi wa maji baada ya Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuchimba kisima chenye uwezo wa kuzalisha lita 13,00 kwa saa na kujenga tanki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita 135,000 kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo.
Akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kümeleta manufaa makubwa kwa wananchi wa maeneo ya Ormekeke, Nasipaoriong na Olduvai yaliyopo hifadhi ya Ngorongoro ambao kipindi cha kiangazi walilazimika kuhamishia mifugo maeneo ya mengine kufuata maji
“Mradi huu tuliuanza kwa kuwashirikisha wananchi ikiwa ni utekelezaji wa kuboresha mahusiano ya NCAA na jamii kwa kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ambalo moja wapo ni maji, umeshakamilisha na kitongoji cha Ormekeke wameanza kutumia maji, rai yangu kwa wananchi ni kulinda na kusimamia miundombinu ya mradi huu kupitia kamati za maji na mazingira ambazo wameshaziunda” alisema Kamishna Badru.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ormekeke Bw. Oreteti Olenjorio ameeleza kuwa eneo la kitongoji hicho ni kame na halina chanzo chochote cha maji hivyo uamuzi wa Serikali kupitia mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kuchimba maji ni msaada mkubwa kwa matumizi ya wananchi na mifugo na kuahidi kulinda miundombinu ya mradi huo kupitia jumuiya za maji na kuzingatia sheria za hifadhi.
Kwa mujibu wa Msimamizi wa Mradi huo Mhandisi Godlove Sengele pamoja na mradi huo kunufaisha wananchi na mifugo yao pia utahudumia Makumbusho ya Olduvai, Leakey Camp, Mtui Camp, Nyumba za Maaskari pamoja na jamii ambayo imejengewa vituo vinne vya kuchotea maji na vituo vitatu vya kunyweshea mifugo.










Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...