Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imeendesha mafunzo maalum kwa Maafisa Ugani 128 wa Mkoa wa Arusha kwa lengo la kuimarisha uzalishaji endelevu na ubora wa mazao ya kimkakati.

Mafunzo hayo yamefanyika kwa ushirikiano kati ya wataalamu wa COPRA, KILICCERT pamoja na Ofisi ya Mkoa wa Arusha, yakilenga kuwajengea uwezo maafisa ugani katika kusimamia na kushauri wakulima kwa ufanisi zaidi.

Kupitia mafunzo hayo, washiriki wamepata maarifa kuhusu: ✅ Viwango vya Uzalishaji Endelevu

✅ Kilimo bora cha mazao ya ufuta na mikunde

✅ Matumizi ya miongozo ya kilimo endelevu iliyoandaliwa na COPRA

✅ Uzingatiaji wa ubora wa mazao kulingana na mahitaji ya soko

Lengo kuu la COPRA ni kuhakikisha mazao yanayozalishwa yanakidhi viwango vya kitaifa na kimataifa, hivyo kuongeza ushindani wa wakulima katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Hatua hii inaonesha dhamira ya COPRA katika kuinua sekta ya kilimo kwa kuimarisha maarifa ya maafisa ugani ambao ni kiungo muhimu kati ya wataalamu na wakulima mashinani.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...