Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma .

Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Dodoma Dkt Frederick Sagamiko amesema kuwa kwa kushirikiana na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wako mbioni kuanzisha kituo atamizi ili kuwajenga vijana,wanawake na wenye ulemavu katika shughuli za kibiashara ili kuleta tija ya Mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri.

Dkt Sagamiko ameyasema hayo leo Februari 11,2026 Jijini Dodoma wakati akifungua Mafunzo ya utoaji mikopo kwa Vikundi ya asilimia 10 kwa kutumia mfumo jumuishi inayoratibiwa na Halmashauri na Benki ya CRDB Foundation.

Pamoja na kuwataka washiriki hao kuwa mabalozi kwa makundi mengine kujua kuwa fedha hizo wanaweza kuzipata lakini ni vema kufuata taratibu muhimu ikiwemo taarifa sahihi za eneo la biashara na kukwepa udanganyifu kama vile kuweka watu wasio sahihi katika kikundi ikiwemo Watumishi wa Umma ambao sio wanufaika.

"Kwa kushirikiana na wenzetu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela tunakuja kuanzisha kituo atamizi kwaajili ya makundi ya vijana,wanawake na wenye ulemavu kwaajili ya kuwajenga kwenye shughuli mbalimbali za kibiashara ili tuone tija ya mikopo hii ya asilimia 10".

Aidha ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa mshirika mzuri katika utekelezaji shughuli za mikopo kwani hadi kufikia Disemba 2025 Halmashauri ilipeleka Benki Shilingi milioni 434,984,000.00 ili kukopesha vikindi 20 ambavyo vimekidhi vigezo, ambapo hadi sasa vikundi hivyo 20 ikiwemo vya vijana 8,wanawake vi 4,na wenye ulemavu 8 vimekwisha patiwa mikopo yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya CRDB Foundation Bi Tully Mwambapa amesema kuwa mpaka sasa maombi ya vikundi 129 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu yamepitishwa katika uchambuzi huku yakiwa na thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni Moja.

"Vikundi 58 vimethibitishwa na benki kuwa vina sifa za kupewa mikopo ya asilimia 10 vikiwa na thamani ya jumla ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.1, kati ya vikundi hivyo, 32 tayari vimeshapatiwa mikopo yenye jumla ya thamani ya Milioni 584, 785 elfu, vikundi 13 vyenye thamani ya shilingi Milioni 199,497 elfu, vimekamilisha mchakato na kwa sasa viko katika hatua ya mafunzo kabla ya kupatiwa mikopo"

Akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya wana vikundi wote na wanufaika wanaopata mafunzo hayo ya kupata fedha za mikopo ya asilimia 10 Magida Chimija amewataka vijana kutokuwa na mtazamo tofauti juu upataji wa mikopo hiyo kwa kudhani kuwa inatolewa kwa kufahamiana bali ni kwa kufuata taratibu na kukidhi vigezo kwani mikopo hii ni kwaajili ya wote wanaokidhi vigezo.

"Tuwe mabalozi wazuri tuwawlekeze wenzetu huko nje,kuwa ni kweli kabisa mikopo hii haina kujuana ni kufuata utaratibu uliowekwa ndipo utaweza kuifikia hii mikopo na hata kama utapewa chini ya kile ulichohitaji chukua tu kwani Benki ipo kila siku".

Tayari Halmashauri imehamisha Shilingi Milioni 183 kwenda Benki ya CRDB kwaajili ya kukopesha vikindi 13 vilivyokidhi vigezo vikiwemo vya Wanawake 5,Vijana 7 na Wenye Ulemavu 1 kutoka kata ya Ng'hong'ona, Hombolo Bwawani,Hombolo Makulu,Nzuguni,Viwandani ,Msalato na Kiwanja cha Ndege.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...