Balozi wa Italia nchini Tanzania, Giuseppe Sean Coppola, amesema kuwa Italia inaadhimisha toleo la 10 la Siku ya Ubunifu wa Italia Duniani, tukio linalolenga kuonesha mchango wa nchi hiyo katika ubunifu wa kimataifa.
Amesema mpango huo umeanzishwa na Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Wizara ya Utamaduni ya Italia, ukiwa na lengo la kukuza ubunifu unaochangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi duniani.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Balozi Coppola alieleza kuwa Italia ni miongoni mwa mataifa vinara katika ubunifu wa bidhaa, akitaja mji wa Milan kuwa kitovu cha ubunifu barani Ulaya na duniani kwa ujumla.
Kwa mwaka huu, maadhimisho hayo yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Kubuni upya: kurejesha, kuboresha na kubadili mawazo, maeneo na mahusiano.”
Maonesho hayo yanafanyika katika ukumbi wa Rangy Gallery, yakihusisha mradi wa pamoja wa utengenezaji wa vioo kati ya Shanga uliopo Arusha na eneo la Murano nchini Italia.
Mradi huo unahusisha wataalamu wa vioo kutoka Murano waliokuja Tanzania kufundisha mbinu za kisasa za utengenezaji wa bidhaa za mikono. Bidhaa hizo hutengenezwa kwa kutumia taka (recycling), hatua inayochangia uhifadhi wa mazingira.
Aidha, Shanga ni taasisi inayowaajiri watu wenye ulemavu, hivyo kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya kijamii na kuwainua kiuchumi.
Katika kuimarisha ubunifu huo, Balozi Coppola alibainisha kuwepo kwa ushirikiano na Nelson Mandela African Institution of Science and Technology, unaolenga kulinda haki miliki za wabunifu.
Maonesho hayo pia yanajumuisha bidhaa za vioo kutoka Venice, jiji lenye historia ya zaidi ya miaka 1,000 katika utengenezaji wa vioo, pamoja na taa za kisasa kutoka kampuni ya Potcerini.
Balozi huyo alisisitiza kuwa ubunifu wa Italia unalenga kuunganisha uzuri na matumizi bora (comfort), huku ukimweka mwanadamu katikati ya kila bidhaa inayobuniwa.
Amewahimiza Watanzania kutembelea maonesho hayo yanayoendelea mwezi mzima wa Aprili, pamoja na kuunga mkono bidhaa za ubunifu na miradi ya kijamii kama Shanga.
Akizungumzia mafanikio ya mradi huo, Balozi Coppola alisema kuwa mapokezi yake katika Murano yalikuwa chanya, huku mafundi wawili wabobezi wa utengenezaji vioo wakifika Tanzania kushiriki mafunzo na kubadilishana ujuzi.
Aliongeza kuwa wadau wa sekta ya ubunifu wameunga mkono mradi huo, wakiuona kama daraja muhimu la kuimarisha uhusiano wa watu kwa watu (people-to-people connection), wenye manufaa makubwa kijamii na kiuchumi.
Kwa ujumla, ushirikiano huo unaendelea kuleta matokeo chanya katika kukuza sanaa, ubunifu na kuimarisha mahusiano ya kimataifa kati ya Italia na Tanzania.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...