Na Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Afya, Dk Florence Samizi amewataka watanzania kuwekeza kwenye miundombinu ya afya ili kusogeza huduma za matibabu karibu na wananchi.
Naibu Waziri ameipongeza hospitali ya E.M ya Kigamboni kwa uwekezaji mkubwa iliyofanya kwenye mtambo wa kisasa wa uchunguzi wa magonjwa CT SCAN na huduma za usafishaji wa damu (Dialysisi) ambao unasaidia kupunguza rufaa zisizo za lazima.
Alitoa pongezi hizo jana Dar es Salaam na wakati wa uzinduzi rasmi wa mashine ya kusafisha damu na mashine ya uchunguzi wa afya CT SCAT ya hospitali hiyo iliyoko kata ya Mjimwema Kigamboni.
Alisema uwekezaji kama huo unasaidia jitihada za serikali kupeleka huduma karibu na wananchi na kuepusha muda na gharama za wananchi kufuata huduma hizo maeneo ya mbali na maeneo wanakoishi.
“Kwaniaba ya Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa napenda kuwapongeza kwa dhati kabisa kwa uwekezaji huu, nilipofika pale nje nilimwambia msaizidi wangu kumbe kitu chenyewe ni kikubwa hivi, nawapongeza sana kwa uongozi mkubwa na kutimiza ndoto na kuwa na wataalamu wazuri maana ungewekeza bila wataalamu isingesaidia sana,” alisema
Alisema uwekezaji uliofanywa na hospitali ya E.M unaonyesha dhamira ya dhati ya kuokoa maisha ya watanzania kupata tiba sahihi na kwa wakati.
“Kama alivyosema Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hii uwekezaji huu umegharimu shilingi bilioni 10 si pesa kidogo ni uwekezaji mkubwa sana tena umefanywa na mtanzania mzawa kusaidia juhudi za serikali kuhudumia watanzania,nawapongeza wote kwa kutimiza haya maono,” alisema
Alisema ili mtu aweze kufanyakazi vizuri lazima awe na afya njema hivyo serikali itaendelea kuwekeza kwenye sekta ya afya kuhakikisha taifa lake linakuwa na wananchi wenye afya.
“Kwa dhati kabisa nampongeza Rais Samia kwa kuwekeza kwenye sekta ya afya, ndani ya miaka minne tu amewekeza zaidi ya trilioni sita ambazo zimeenda kwenye miradi ya ujenzi wa hospitali na zahanati, ameweza kujenga hospitali 119, vituo vya afya 649 na zahanati 2,700 na kuweka vifaa tiba vya kisasa na ameajiri watumishi wa afya,” alisema
“Huduma kama uchujaji wa damu ni muhimu sana kwa wananchi wanaosumbuliwa na figo hivyo huduma hiyo itawasaidia sana wananchi kuchuja damu na kuendelea na maisha yao, huduma hizi tumezoea kuzipata nje ya nchi sasa leo hii mzawa amezileta Kigamboni,” alisema
“Nasikia ni ya kwanza Kigamboni kutoa huduma hii napenda kuwaambia wananchi hakuna haja ya kwenda mbali kutafuta huduma mfike hapa E.M kupata huduma hizo badala ya kuhangaika kwenda mbali,” alisema
Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk Egna Makwabe alisema wamekuwa wakipata wagonjwa kutoka nchi za Congo DCR, Zambia, Malawi, Comoro, Burundi Rwanda, Benin, Ghana, Nigeria, Kenya, Urusi china na Marekani .
“Ujio wa wagonjwa kutoka nje ya nchi ulitushangaza sana tunakiuliza je wanakuja kwasababu ya eneo tulilopo au ninini hasa kimewavutia kuacha hospitali zote kuja kwetu tukagundua kuwa ni imani yao kutokana na huduma tunazotoa,” alisema
Alisema kwa sasa hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wa nje wastani wa 300 kwa siku na kwamba kwa sasa wanamadaktari bingwa bobezi wauguzi na wataalamu wa maabara.
Alisema E.M itashirikiana na serikali kuhakikisha bima ya afya kwa wote inawanufaisha wananchi wanapougua wasilazimike kutoa fedha kupata matibabu na kwamba walishiriki kutoa maoni kwenye uandaaji wa bima ya afya kwa wote.
Alisema wanatoa huduma za kuwaona wagonjwa wa nje, wanaolazwa, huduma za upasuaji, huduma za matibabu ya mgongo, mfumo wa fahamu na mifupa, huduma za maabara na geologia, huduma za uangalizi maalum na huduma za kibingwa za figo na saratani.
Alisema hospitali imewekeza kwenye huduma za kuchuja damu, mitambo ya kuchunguza magonjwa kama CT SCAN na upasuaji wa kisasa kwa njia ya matunda na karibuni wataanzisha huduma za macho .

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...