-Watanzania waaswa kulinda amani

Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Machi 21, 2026 ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na waumini wa dini ya Kiislam kwenye Swala ya Eid El-Fitri katika Msikiti Mkuu wa BAKWATA (Mfalme Mohamed VI), Kinondoni, jijini Dar es Salaam.


Ibada hiyo ya kitaifa iliyoongozwa na Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Bin Zubeir, inayofanyika mara baada ya kumalizika kwa siku 30 za mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan Machi 20, 2026



Pia ibada ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule.



Katika ibada hiyo Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Bin Zubeir, amehimiza amani, umoja na mshikamano kwa waumini wa kiislam na watanzania kwa ujumla.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...