Na. Mwandishi Wetu.

Awamu ya Tatu ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka maarufu kama Mwendokasi katika Barabara ya Nyerere kuelekea Gongolamboto na maeneo yaJirani sasa umefikia asilimia 99 kwa ujenzi wa Vituo vya Mabasi Pamoja na Barabara za zege.

Akizungumza kuhusu maendeleo ya awamu hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Bi. Delphina Pweleza amesema kuwa ujenzi wa awamu hiyo ya tatu ya BRT uligawanyika katika Lot 2 yaani ujenzi wa miundombinu ya Barabara na Vituo vyake ambao mpaka sasa umefikia asilimia 99% huku Lot ya 2 inayohusisha ujenzi wa Karakana, Kituo Kikuu cha Airport na kituo mlishi cha Banana ikiwa kwenye hatua za awali.

“Kwa sasa ujenzi wa miundombinu ya barabara na vituo umekamilika kwa asilimia tisini na tisa (99%) na matarajio ya kukabidhiwa ikiwa ni mwishoni mwa mwezi April 2026” Alisema Bi. Pweleza.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa Gongolamboto Jijini Dar es Salaam wamesema mradi huo utakapoanza kufnya kazi utakuwa mkombozi mkubwa katika usafiri wa umma kwani wameusubiri kwa muda mrefu.

“Tunaishukuru Serikali ya Dkt Samia kwa kuendelea kujenge miundombinu ya kimkakati kama hii ambayo lengo lake kubwa ni kutuondolea kero ya usafiri sisi wakazi wa Gongolamboto, Pugu, KIsarawe na maeneo ya Jirani” Alisema Hamad Shelukindo Mkazi wa Pugu Kajiungeni JIjini Dar es Salaam.

Naye Anselim Obeid wa Ukonga amesema mradi huo utakapoanza utawasaidia sana wakina mama na wanaunzi ambao mara nyingi wamekuwa wakihangaika na usafiri wa umma usio wa uhakika.

Awamu ya tatu ya mradi wa BRT kuelekea Gongolamboto inahusisha tawi lingine la Barabara linaloanzia kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Kariakoo Gerezani kupitia mitaa ya Lindi, Shaurimoyo na Uhuru hadi Buguruni inapoungana na Barabara ya Nelson Mandela na kujiunga na Barabara ya Nyerere kwenye makutano ya TAZARA ikiwa na urefu wa kilomita 23.6 ikiunganishwa na Awamu ya Kwanza na ya Pili ya mradi katika Vituo Vikuu vya Kariakoo - Gerezani na Kivukoni.

Aidha awamu ya tatu ujenzi unajumuisha barabara pekee za Mabasi (exclusive BRT lanes), barabara za magari binafsi, njia za waenda kwa miguu pamoja na baiskeli zenye jumla ya urefu wa kilomita 23.6, Vituo Vikuu na vidogo vya mabasi, karakana pamoja na vituo mlishi.

Ujenzi wa miundombinu ya Awamu ya Tatu ya Mradi wa DART unatekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Hali ya Usafiri katika Jiji la Dar es Salaam (DUTIP).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...