NAIROBI, KENYA. Kampuni ya Kerry Group, kinara wa kimataifa katika masuala ya ladha na lishe, imezindua ripoti ya Kenya 2026 Taste Charts, ikionyesha mabadiliko makubwa katika chaguo za ladha za watumiaji barani Afrika. Ripoti hizi mpya, zinazohusisha nchi 78 barani Afrika zikiwemo Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, na Zambia, zinaonyesha kuwa watumiaji wa Afrika sasa wanazidi kuhama kutoka kwenye ladha za kawaida za vyakula vya msingi na badala yake wanatafuta ladha zilizo na mchanganyiko mpana, zilizo maalum zaidi, zenye utofauti mkubwa na uzoefu unaofanana na ule wa “cocktail” katika vyakula na vinywaji vya kila siku.
Ripoti ya Taste Charts 2026 imetayarishwa kwa msaada wa timu pana ya wataalamu zaidi ya 1,200 wa sayansi, wataalamu 100 wa ubunifu wa ladha (flavourists), wataalamu 70 wa sanaa ya chakula, pamoja na zaidi ya wataalamu 250 wa masoko na uchambuzi wa mwenendo wa watumiaji.
Kadiri matarajio ya watumiaji yanavyozidi kubadilika na kuwa tofauti, Taste Charts 2026 imepanua makundi yake kutoka matano hadi saba katika ukanda huu. Makundi hayo yanajumuisha: vinywaji vya viburudisho, pombe na vile vinavyochochewa na ladha za pombe, chai, kahawa na kakao, vitafunwa vyenye ladha ya chumvi, vyakula vitamu, supu na virutubisho, pamoja na nyama, milo kamili na virutubisho. Mtazamo huu mpana unaonyesha namna kustarehe na kujali afya, mila na mtindo mpya, pamoja na ushawishi wa kimataifa na utambulisho wa ndani vinavyochangia zaidi maamuzi ya ladha.
“Kile tunachokiona kinaonyesha mabadiliko ya msingi katika namna watumiaji barani Afrika wanavyotumia vyakula na vinywaji kwa sasa. Tunashuhudia mwelekeo wa kuhama kutoka kwenye ladha za jumla na kuelekea kupata uzoefu maalum na wenye tabaka nyingi za ladha. Watumiaji hawataki tena ladha ya machungwa kwa ujumla; wanataka ladha maalum kama ukali wa Tangawizi au uchachu wa kipekee wa Ukwaju,” alisema Regis Manyange, Mkurugenzi wa Biashara Afrika Mashariki wa Kerry Group.
“Kwa kuyakusanya maarifa haya na msaada wa matumizi kwa vitendo pamoja na upatikanaji wa sampuli kwa haraka kupitia KerryNow™, tunawasaidia wateja wetu kugeuza mawazo yao kuwa bidhaa halisi kwa ufanisi zaidi na kuendana na kasi ya mabadiliko ya ladha za watumiaji.”
Uburudishaji Kufuata Tabia Maalum: Mwelekeo wa Ladha Mahususi
Matunda yanayotumika kama viburudisho yanaendelea kuongoza kutumika kwenye ubunifu wa vinywaji, lakini mahitaji ya ladha halisi yanaongezeka. Ingawa ladha za asili kama machungwa na limao bado zinaongoza kwa kiasi cha matumizi, ripoti zinaonyesha kuongezeka kwa mahitaji ya aina maalum na za kisasa zaidi. Katika Rwanda, Uganda, na Zambia, ladha ya Tangawizi imepanda na kuwa ladha inayokua kwa kasi zaidi katika vinywaji vinavyoburudisha, ikiendana na mahitaji ya kimataifa ya vinywaji vyenye ladha safi na tamu ya asili. Wakati huo huo, Tanzania inaonyesha fahari ya ladha za asili, ambapo Ukwaju umetajwa kuwa ladha mpya inayochipukia kwa kasi, ishara ya kurejea kwenye ladha zenye ukali, uchachu na za asili za ndani.
Tamu na Kali: Kuibuka kwa Ladha ya “Swicy”
Mchanganyiko wa ladha tamu na kali unaendelea kupata umaarufu kadiri watumiaji wanavyotafuta uzoefu wenye nguvu, tofauti na unaoweza kutumiwa kwa pamoja na jamii. Mwelekeo huu unaonekana zaidi Kenya, ambapo ubunifu wa ladha za “Swicy” unaongoza katika vinywaji vinavyochochewa na ladha za pombe, ikiwa ni pamoja na mchanganyiko kama Mango Chilli. Katika ukanda mzima, uhitaji wa ladha hizi zenye ukali uliokadiriwa inaonekana pia katika vitafunwa vyenye chumvi, ambapo matumizi ya pilipili ya kawaida yanabadilika na kuwa mifumo ya viungo yenye tabaka nyingi za ladha.
Zaidi ya Ukali Pekee: Ladha Zenye Tabaka Nyingi, Ulimwengu Ukikutana na Ladha za Ndani
Watumiaji wanazidi kuhama kwenye ladha za ukali wa aina moja na kuelekea ukali uliokadiriwa na wenye tabaka nyingi. Afrika kwa ujumla, mchanganyiko wa viungo unaotokana na ‘paprika’ unaongezeka katika vitafunwa, mchuzi, nyama za kuchoma na milo iliyo tayari, ukitoa ladha nzuri, tamu na harufu nzuri inayochochewa na utamaduni wa vyakula vya mitaani. Mwelekeo huu unaunga mkono matumizi ya mifumo lukuki ya viungo inayotoa ladha pana badala ya ukali pekee. Kwa Tanzania na Kenya, mabadiliko haya yanaonekana pia kwenye vitafunwa, ambapo ladha ya ‘Salted Caramel’ imeunganisha ladha ya chumvi na utamu kuleta uzoefu wa kifahari na ladha nyingi tofauti.
Athari ya “Mocktail”: Ladha za Pombe katika Vinywaji Visivyo na Pombe
Mwelekeo mwingine mkubwa katika ukanda huu ni kuongezeka kwa matumizi ya ladha zinazochochewa na vinywaji vya pombe katika vinywaji visivyo na pombe. Watumiaji wanatafuta ubunifu na usasa wa utamaduni wa ‘cocktail’ bila kutumia pombe. Ladha ya ‘Mojito’ sasa ni miongoni mwa ladha tatu zinazoibuka kwa kasi Tanzania na Rwanda. Vivyo hivyo, ladha ya ‘Piña Colada’ imeingia kwenye ladha tano zinazokua kwa kasi zaidi Uganda na Zambia, ikionyesha shauku ya watumiaji ya ladha za kitropiki na zenye utamu wa ‘cream’ katika matumizi ya kila siku.
Kubadilisha Maarifa kuwa Hatua
Ripoti Taste Charts 2026 sasa inaungwa mkono na jukwaa la kidijitali linalorahisisha matumizi yake kutoka uchambuzi mpaka utekelezaji: KerryNow™. Kwa mara ya kwanza, wateja wanaweza kupata moja kwa moja orodha ya ladha, kuagiza sampuli za ladha zinazotajwa kwenye Taste Charts, na pia kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa Kerry Group kuhusu matumizi ya ladha hizo katika bidhaa mbalimbali.
Kwa taarifa zaidi tafadhali soma ripoti iliyoambatishwa hapa.
-MWISHO-
Kuhusu Kerry
Kerry Group ni mshirika anayeongoza duniani katika sekta za ladha na lishe kwa masoko ya vyakula, vinywaji na bidhaa za dawa. Kampuni hii hushirikiana na wateja wake kubuni bidhaa zenye ladha bora, lishe iliyoboreshwa na utendaji mzuri zaidi, huku ikichangia pia katika kulinda mazingira na kuleta athari chanya duniani. Kwa taarifa zaidi, tembelea tovuti ya Kerry.



.jpg)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...