Na Mwandishi wetu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha jumla ya Shilingi trilioni 2.39 kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Elimu kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ikiwa ni hatua inayolenga kuimarisha maendeleo ya sekta ya elimu, sayansi na teknolojia nchini.

Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo Kwa mwaka wa fedha 2026/27 Bungeni jijini Dodoma, Prof. Mkenda amesema fedha hizo zitatumika kugharamia matumizi ya kawaida pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye lengo la kuboresha ubora wa elimu nchini.

Kwa mujibu wa makadirio hayo, Wizara ya Elimu (Fungu 46) inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 2,394,423,829,000, ambapo Shilingi 697,841,881,000 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya Wizara.

Kati ya fedha hizo za matumizi ya kawaida, Shilingi 648,082,352,000 zitatumika kulipa mishahara ya watumishi wa Wizara, huku Shilingi 49,759,529,000 zikitengwa kwa ajili ya matumizi mengineyo ya uendeshaji wa shughuli za kila siku za Wizara.

Aidha, kwa upande wa miradi ya maendeleo, Wizara imeomba jumla ya Shilingi 1,696,581,948,000, ambapo kati ya hizo Shilingi 1,337,249,000,000 ni fedha za ndani na Shilingi 359,332,948,000 ni fedha kutoka kwa washirika wa maendeleo.

Vilevile, kupitia Tume ya Taifa ya UNESCO (Fungu 18), Wizara imeomba kuidhinishiwa Shilingi 3,866,993,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ambapo Shilingi 1,335,020,000 zitatumika kwa mishahara na Shilingi 2,531,973,000 kwa matumizi mengineyo ya uendeshaji.

Kwa ujumla, Wizara ya Elimu na Tume ya UNESCO imeomba Bunge kuidhinisha jumla ya Shilingi 2,398,290,822,000 kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027.

Prof. Mkenda amehitimisha hotuba yake kwa kutoa shukrani kwa Spika wa Bunge, Waheshimiwa Wabunge na wadau wote kwa ushirikiano wao, akisisitiza kuwa bajeti hiyo itachochea kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sekta ya elimu nchini na kuongeza ubora wa huduma za elimu kwa wananchi.


Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...