TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imemkabidhi rasmi fomu za kugombea ubunge wa jimbo la Isimani kwa Emanuela Mtatifikolo Kaganda, kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika Juni 1 mwaka huu.
Zoezi hilo limefanyika katika ofisi za tume zilizopo Ihemi chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi jimbo la Isimani, Caroline Ang’weni Otieno.
Emanuela alikabidhiwa fomu hizo akisindikizwa na viongozi mbalimbali wa wilaya akiwemo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa Vijijini, Costantino Kihwele ambapo baada ya kupokea fomu, Emanuela aliwashukuru viongozi na wanachama wote kwa kujitokeza, akisisitiza kuwa ana dhamira ya kutoa mchango chanya kwa maendeleo ya jimbo la Isimani.
Katika hotuba yake, aliwatambua viongozi wa jumuiya zote za chama ikiwemo jumuiya ya wazazi, vijana na UWT, pamoja na madiwani na viongozi wa ngazi mbalimbali.
Aliweka wazi kuwa, licha ya jimbo hilo kupitia kipindi kigumu kutokana na msiba wa aliyekuwa mbunge, wananchi wamethibitisha umoja na mshikamano mkubwa.
Emanuela alitoa shukurani za pekee kwa uongozi wa chama kuanzia ngazi ya shina hadi taifa, kwa kusimamia mchakato wa uteuzi kwa haki na uwazi na alipongeza pia wagombea wenzake walioshiriki mchakato huo na kuonyesha umoja baada ya kukamilika kwa uteuzi.
Aidha, alisisitiza kuwa jimbo la Isimani tangu kuanzishwa kwake limeongozwa na kiongozi mmoja, marehemu William Vangimembe Lukuvi, ambaye alifanya kazi kubwa ya kuliletea maendeleo.
Aliahidi kuendeleza misingi ya maendeleo iliyoachwa na kiongozi huyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Costantino Kihwele, alimpongeza Emanuela kwa kuteuliwa na kamati kuu kuiwakilisha CCM kwenye uchaguzi huo mdogo.
Aliwahimiza wanachama kuendelea na umoja na maandalizi ya kampeni, akieleza kuwa chama kitafanya kampeni za kidiplomasia na za ushahidi wa kazi zilizofanyika.
Kihwele pia aliwapongeza wagombea wengine waliokuwa kwenye mchakato wa awali kwa kuonyesha uzalendo na kukubali matokeo, akiahidi kuwa watashirikishwa kikamilifu katika kampeni zitakapoanza rasmi.
Viongozi na washiriki wa mkutano huo walionyesha hamasa ya pamoja, huku wakiahidi kumpa mgombea wao ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa Juni 1.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...