.jpeg)
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya NIC Insurance imewahimiza wamiliki wa vyombo vya moto nchini kuhakikisha wanakata bima ili kujikinga na athari za kifedha zinazoweza kujitokeza pindi yanapotokea majanga au ajali.
Wito huo umetolewa na Afisa Bima wa NIC Insurance, Iman Mollel, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la kampuni hiyo kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mollel amesema NIC Insurance imeendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa kuhakikisha madai ya fidia kwa magari yaliyoharibika kiasi cha kutotengenezeka (total loss) yanashughulikiwa kwa haraka, ambapo malipo hufanyika ndani ya siku saba baada ya mteja kukamilisha nyaraka zote zinazohitajika.
Amesema kampuni hiyo inatoa bima kwa aina mbalimbali za vyombo vya moto, ikiwemo magari binafsi, magari ya biashara, magari ya mizigo, mabasi na magari ya abiria, bajaji pamoja na pikipiki, ili kuhakikisha wamiliki wake wanapata kinga dhidi ya hasara zinazoweza kujitokeza.
Aidha, Mollel amesema NIC Insurance imeweka huduma za kidijitali zinazowawezesha wateja kupata huduma za bima kwa njia ya mtandao, hatua inayolenga kupunguza gharama na muda wa kusafiri kufuata huduma katika ofisi za kampuni hiyo.



.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...