Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndg. Abdi Mahmoud Abdi, amesema changamoto zinazowakabili wananchi zinapaswa kutatuliwa kuanzia katika ngazi zote za maamuzi ndani ya Chama, kuanzia matawi hadi Afisi Kuu ya CCM.
Ndg. Abdi ameyasema hayo leo, Septemba 13, 2026, alipowasili katika Tawi la CCM Kivunge, Jimbo la Kijini, ambapo alizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wajumbe wa Kamati za Siasa.
Amesema ushiriki wa wanachama katika vikao mbalimbali vya Chama ni muhimu katika kuimarisha umoja na mshikamano kati ya viongozi na wanachama, sambamba na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Chama.
Aidha, amesema Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, anaendelea kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo, ikiwemo kuhakikisha wananchi wanapata ufumbuzi wa changamoto zinazohusu huduma za kijamii.
Amezitaja huduma hizo kuwa ni pamoja na elimu, afya, maji safi na salama, pamoja na ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya barabara.
Katika ziara hiyo, Ndg. Abdi pia alimtembelea na kumjulia hali Ndg. Fatima Mtwana Ame nyumbani kwake Kivunge, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza mshikamano, upendo na kujali wanachama wa CCM.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...