Na George Maziku, Mbogwe
DIWANI Kata ya Bukandwe, iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita Paulo Raphael Sahani amewalaumu wazazi katika shule ya msingi Kanegere, iliyopo kijiji cha Kanegere wilayani humo, kwa kuitelekeza shule hiyo na kusababisha uchakavu mkubwa.
Diwani huyo ametoa lawama hizo jana Alhamisi, Septemba 24, katika sherehe za mahafari ya 22 ya wanafunzi waliohitima darasa la saba mwaka huu, ambapo diwani huyo alikuwa mgeni rasmi.
Alisema kuwa wazazi na wananchi wa kijiji cha Kanegere wameacha kujitolea kuchangia maendeleo ya shule yao, badala yake jukumu hilo wamewaachia wawekezaji wa sekta ya madini waliopo kijijini hapo, ambao hatahivyo diwani huyo alidai hawasomeshi watoto wao katika shule hiyo.
"Sisi viongozi, walimu, kamati ya shule na wazazi wa shule hii kwa ujumla wetu tumefeli kabisa kuihudumia shule yetu. Tumeitelekeza kabisa na kuifanya ichakae na kukosa hadhi ya kuitwa shule inayotegewa kutoa elimu bora kwa watoto wetu. Tumewaachia wawekezaji jukumu la kuhudumia shule yetu lakini wao hawana watoto wanaosoma hapa", alisema diwani Sahani.
"Lazima tubadilike, tuanze kuchangia shule yetu sasa. Wazazi wa watoto wanaohitimu darasa la saba wachangie angalau mfuko mmoja wa saruji kwa ajili ya maendeleo ya shule hii, haiwezekani mtoto akae hapa miaka saba halafu aondoke hivi hivi bila kuchangia chochote, na katika kipindi hicho inawezekana ameharibu miundombinu ya shule kama milango, madirisha au ameharibu bati kwa kutupa mawe kwenye paa, hii siyo sawa hata kidogo", alifafanua Sahani.
Sahani alisema kuwa kuanzia mwakani kutakuwa na mabadiliko makubwa ambapo kila mzazi wa mtoto anaehitimu darasa la saba katika shule hiyo atatakiwa kuchangia angalau mfuko mmoja wa sementi kwa ajili ya ukarabati na umaliziaji wa majengo ya shule ya Kanegere.
"Tuanze mwakani kwasababu tutakuwa na wahitimu wengi, kwa maana wanafunzi waliopo leo darasa la sita na la tano watahitimu pamoja. Tunaweza kuwa na wahitimu kati ya 300 mpaka 400, hivyo tunaweza kupata mifuko 300 mpaka 400 ya saruji na kuweza kumalizia baadhi ya majengo yetu na kufanyia ukarabati mengine", alisisitiza diwani huyo.
Wakati huo huo diwani huyo amewatolea wito watu wote waliosoma shule ya msingi Kanegere kuikumbuka shule hiyo kwa kuchangia maendeleo yake.
Diwani huyo ambaye pia alihitimu darasa la saba katika shule hiyo mwaka 2004, aliahidi kuwatafuta na kuwaunganisha watu wote waliohitimu shuleni hapo kati ya mwaka 2004 mpaka 2010 ili waweze kuchangia ujenzi na ukarabati wa shule yao kama shukrani kwa mafanikio yao ya leo.
"Napenda kutangaza kupitia mahafari haya kwamba katika mahafari ya mwaka ujao, wahitimu wote wa shule hii wa kuanzia mwaka 2004 mpaka 2010 ndio watakuwa wageni rasmi na mimi ndiye mwenyekiti wa kamati ya maandalizi hayo, nitawatafuta kila mahali walipo na kuwashawishi wachangie yao", alibainisha diwani huyo.
Aliongeza, "Lazima tufanye kazi mchana na usiku ili kurejesha haraka hadbi ya shule yetu, inatubidi turudishe shukrani zetu kwenye shule iliyotusomesha. Inakuwaje tutoe fungu la kumi kanisani halafu tushindwe kuchangia shuleni", alihoji diwani huyo.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba shuleni hapo mwaka huu walielezea furaha yao pamoja na matumaini yao ya baadaye.
"Najisikia vizuri na nina furaha sana kufikia hatua hii. Malengo yangu ni kuendelea na masomo ya sekondari na chuo ili niweze kutimiza ndoto zangu za kuwa rubani wa ndege", alisema Janeth Emmanuel (14) mmoja wa wahitimu wa mwaka huu.
Nae mhitimu mwingine Gaudencia William (13) alisema kuwa ana imani kubwa kwamba atafaulu mtihani wake wa darasa la saba na kuendelea na masomo ya sekondari na hatimaye kutimiza lengo lake la kuwa daktari wa binadamu.
"Mimi nataka kuwa daktari wa kutibu watu, naamini nitafaulu kwenda sekondari na nikifikaa huko nitasoma masomo ya sayansi kwasababu nayapenda na ninayaweza", alijigamba Gaudencia.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...