NA MWANDISHI WETU, TANGA
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kiongozi mwenye uwezo mkubwa ndani ya Bara la Afrika, mvumilivu na mchapakazi.
Kihongosi ameyasema hayo wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Tanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Lamore, ikiwa ni hitimisho la ziara yake mkoani humo ya kukagua uhai wa Chama pamoja na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2025–2030.
Amesema Rais Samia ameithibitishia dunia kuwa wanawake wanaweza kuongoza nchi kwa ufanisi na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya muda mfupi.
“Rais Samia ni kiongozi mwenye uwezo mkubwa, si Tanzania pekee bali pia ndani ya Bara la Afrika. Ni mvumilivu, mchapakazi, mwenye hofu ya Mungu, anayesikiliza na kutatua kero za wananchi,” amesema Kihongosi.
Amesema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, ikiwemo mkoani Tanga, ni miongoni mwa ushahidi wa juhudi za Serikali katika kuendeleza maendeleo ya Taifa.
Ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa Bandari ya Tanga, ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Tanga pamoja na ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR).
Aidha, Kihongosi amewataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia katika jitihada za kuwatumikia Watanzania na kuhakikisha Taifa linaendelea kupata maendeleo endelevu.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...