Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo, ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe na kuzindua mradi wa kurasimisha makazi ya wananchi wa Kata ya Hale, unaotekelezwa katika eneo lenye ukubwa wa ekari 4,200.

Mradi huo unalenga kuwawezesha wananchi kupata hati na nyaraka halali za umiliki wa ardhi na makazi yao, hatua itakayosaidia kuongeza usalama wa umiliki wa ardhi pamoja na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe,Wakili.Goodluck Mwangomango amemshukuru Dkt. Akwilapo kwa hatua hiyo yenye tija kwa wananchi, akieleza kuwa utekelezaji wa mradi huo utatoa fursa kwa wananchi kutumia ardhi yao kwa uhakika zaidi katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Aidha, Halmashauri imetoa pongezi na shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga na kupeleka fedha katika Halmashauri ya Korogwe kwa ajili ya kusaidia wananchi katika maendeleo ya sekta ya ardhi.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za ardhi na kuwa na uhakika wa umiliki wa maeneo yao kwa mujibu wa sheria.


Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe,Wakili.Goodluck Mwangomango wakati wa kuzindua mradi wa kurasimisha makazi ya wananchi wa Kata ya Hale, unaotekelezwa katika eneo lenye ukubwa wa ekari 4,200.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe,Wakili.Goodluck Mwangomango akifafanua jambo mbele ya Mgeni rasmi na wageni waalikwa (hawapo pichani).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...