Kijiji cha Kinyamwenda, Kilichopo Mkoani Singida, kimeweka utaratibu wa kuwawajibisha wananchi wanaotumia punda kubeba mizigo bila kuzingatia matumizi ya matandiko maalumu, ikiwa ni hatua ya kupunguza majeraha na maumivu yanayowapata wanyama hao wakati wa ubebaji wa mizigo.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Ndugu. Iddi Ismaili, amesema punda wanatumika kwa kiasi kikubwa katika kubeba mizigo katika eneo hilo, hivyo matumizi ya matandiko ni muhimu kwa kuwa huzuia mzigo kugusa moja kwa moja mwili wa mnyama na kusababisha majeraha.
Amesema matandiko yaliyotengenezwa na kupelekea kijijini hapo na Shirika la INADES Formation Tanzania Tanzania kupitia Mradi wa kuboresha maisha ya jamii kupitia mnyamakazi punda, yamewapa wanakijiji fursa ya kujifunza namna ya kuyatengeneza ili yaweze kupatikana kwa wingi na kutumiwa na watu wengi zaidi.
“Punda Kinyamwenda ni wengi, lakini wakati mwingine wanabeba mizigo bila kufuata utaratibu unaozingatia haki yao, Matandiko haya yanamwezesha punda kubeba mzigo katika hali nzuri bila kuumia."
Katika kuunga mkono hatua hiyo, INADES-Formation Tanzania imekabidhi magunia na kamba kwa vikundi vinavyohusika na ustawi wa punda, kwa ajili ya kutengeneza matandiko yatakayosaidia kupunguza vidonda vinavyosababishwa na msuguano wa mizigo kwenye migongo ya punda.
Daktari wa Mifugo wa INADES Tanzania, Charles Lucas Bukula, amesema lengo la msaada huo ni kuboresha afya na ustawi wa punda ili waweze kuendelea kutumika kwa muda mrefu katika shughuli za uzalishaji na kusaidia wamiliki wao kupata kipato, huku akiwashukuru wafadhili wa shirika hilo, Brooke West Africa, kwa kuendelea kuunga mkono shughuli hizo kwa takribani miaka sita.
Kwa ujumla, ushirikiano kati ya Kijiji cha Kinyamwenda, na Shirika la INADES-Formation Tanzania unalenga kuhakikisha matumizi ya punda yanafanyika kwa kuzingatia ustawi wao, huku hatua za kuzuia majeraha na kuboresha afya ya wanyama hao zikichangia pia kuwalinda kama rasilimali muhimu katika shughuli za kiuchumi za wananchi.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...