Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amefika nyumbani kwa familia ya Marehemu Mama Fatma Karume, Mbweni, Wilaya ya Magharibi “B”, Unguja, leo tarehe 22 Septemba 2026, kutoa pole na rambirambi kufuatia kifo chake. Mama Fatma Karume alikuwa mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar.
Rais Dkt. Mwinyi amesaini kitabu cha maombolezo na kutoa pole kwa wanafamilia, akiwataka kuwa na subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amewaomba wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki kuendelea kumuombea Marehemu Mama Fatma Karume, Mwenyezi Mungu amrehemu na amjaalie makaazi mema Peponi, huku akiwaombea wafiwa subira na moyo wa ustahimilivu.



.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...