Vero Ignatus – Michuzi TV Arusha
KONGAMANO la Kitaifa la Ufuatiliaji na Tathmini linatarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Septemba 22 hadi 26, 2026, likiwakutanisha washiriki kutoka serikalini, taasisi za umma, sekta binafsi pamoja na wadau wa maendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, amesema kongamano hilo litafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Ngurdoto, wilayani Arumeru, na linatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 1,500, huku mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba.
Makalla amesema kongamano hilo litajadili uzoefu, ubunifu na mbinu bora za ufuatiliaji na tathmini, pamoja na namna ya kutumia matokeo ya tathmini katika kuboresha utoaji wa huduma kwa umma na kuhakikisha shughuli za maendeleo zinawanufaisha wananchi.
Amesema ufuatiliaji na tathmini ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo unafanyika kwa ufanisi na matokeo yanayopimika, huku wananchi wakipata fursa ya kutoa ushahidi kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo katika maeneo yao.
Ameongeza kuwa, katika kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050, Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) pamoja na Ajenda ya Umoja wa Afrika 2063, ufuatiliaji na tathmini si zoezi la kiufundi pekee, bali ni msingi muhimu wa kupanga, kutekeleza na kuboresha mipango yenye tija kwa wananchi.
Kwa upande wake, Charlton Meena, Ofisa Mwandamizi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, amesema kongamano hilo limebeba kaulimbiu isemayo, “Kuimarisha Tathmini kwa Maendeleo Endelevu ya Watu.”
Meena amesema washiriki 1,500 tayari wamethibitisha kushiriki kongamano hilo, ambalo litajadili mada mbalimbali zinazolenga kuimarisha mifumo ya kufanya maamuzi inayozingatia ushahidi na data sahihi, kuongeza uwajibikaji pamoja na kuboresha utendaji wa taasisi.
Amesema kongamano hilo pia litatoa fursa kwa wadau kubadilishana uzoefu na kujadili mbinu bora zinazoweza kutumika katika kuimarisha ufuatiliaji na tathmini, ili kuhakikisha maamuzi ya maendeleo yanafanyika kwa kuzingatia taarifa sahihi na matokeo yanayopimika.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...