Na Mwandishi Wetu, Nzega
MWENGE wa Uhuru umezindua mradi wa upanuzi wa mfumo wa kusafisha na kutibu maji unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Nzega Mjini (NUWASA), huku ukielezwa kuwa utasaidia kuimarisha upatikanaji wa maji kwa wananchi.
Mradi huo umezinduliwa leo, Septemba 19, 2026, na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Mhe. Naitapwaki Tukai, mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang'onda.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Tukai amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama, sambamba na kupunguza magonjwa ya mlipuko yanayoweza kusababishwa na ukosefu wa maji.
Amesema mradi huo pia umewawezesha wananchi wa Mji wa Nzega kupata huduma ya maji kulingana na mahitaji na uwezo wao wa kulipia.
“Wananchi wa Mji wa Nzega wanatumia maji kadiri wanavyohitaji kupitia mradi huu. Wananchi wanaweza kulipia kiasi wanachohitaji; wakitaka maji ya Shilingi 3,000 wanapata na wakitaka ya Shilingi 100,000 pia wanapata,” amesema.
Kwa upande wake, Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Salum Yasin Ikinda, amesema mradi umetekelezwa kwa kipindi cha miezi 36 na umejengwa na kampuni ya FABEC Investment Ltd.
Amesema mradi huo umetekelezwa kwa gharama ya Shilingi 620,103,998.30, ambapo hadi sasa mkandarasi ameshalipwa Shilingi 290 milioni.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang'onda, ameipongeza Nzega kwa utekelezaji na ubora wa mradi huo.
“Kutokana na ubora wa mradi huu, hapa panapaswa kulindwa kwa wivu mkubwa ili kuhakikisha unakuwa endelevu kwa maslahi mapana ya jamii ya eneo hili,” amesema Mwang'onda.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...