Na Janeth Raphael - MichuziTv
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kimeiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa umma, kikisema utatuzi wa masuala hayo ni muhimu katika kuboresha mazingira ya kazi, maslahi ya wafanyakazi na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Ombi hilo limetolewa leo Septemba 17, 2026 jijini Dodoma na Kaimu Katibu Mkuu wa TALGWU, Wandiba Ngocho, wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama hicho uliohusisha viongozi wa Serikali pamoja na wajumbe kutoka vyama vya wafanyakazi ndani na nje ya Tanzania. Ngocho amesema miongoni mwa changamoto hizo ni ucheleweshaji wa malipo ya fedha za likizo, ambapo baadhi ya watumishi hupokea stahiki hizo kwa awamu au baada ya muda uliopangwa.
Amesema changamoto nyingine ni ucheleweshaji wa malipo ya posho pamoja na leseni za huduma kwa watumishi wa kada za afya, hali ambayo imekuwa ikiwafanya baadhi ya watumishi kusubiri muda mrefu kabla ya kupata stahiki zao. Pia, TALGWU imeeleza kuwepo kwa ucheleweshaji wa malipo ya stahiki za uhamisho kwa watumishi wanaohamishwa kutoka kituo kimoja cha kazi kwenda kingine.
Kwa upande mwingine, chama hicho kimeomba maboresho katika utekelezaji wa mfumo wa Upimaji Utendaji Kazi (PEPMIS), kikieleza kuwa baadhi ya watumishi wanakabiliwa na changamoto katika matumizi yake. TALGWU pia imeibua suala la miundo ya utumishi na mchakato wa kubadilishiwa kada (re-categorization), ambapo baadhi ya watumishi hukumbana na vikwazo licha ya kuwa na elimu na ujuzi unaohusiana na kada wanazohitaji kuhamia.
Ngocho amesema TALGWU pia imebaini changamoto katika utendaji wa baadhi ya Mabaraza ya Wafanyakazi katika halmashauri na taasisi, hali inayopunguza ufanisi wa ushirikishwaji wa wafanyakazi katika masuala yanayohusu ajira na mazingira yao ya kazi. Chama hicho kimeomba hatua zichukuliwe kuimarisha mabaraza hayo pamoja na kuboresha zaidi mazingira ya kazi na maslahi ya watumishi, hususan wanaofanya kazi katika maeneo ya pembezoni.
Akizungumzia umuhimu wa kushughulikia changamoto hizo, Ngocho amesema utatuzi wake utaongeza morali na ari ya watumishi, hivyo kuchangia ufanisi katika utekelezaji wa majukumu na utoaji wa huduma bora kwa wananchi. Aidha, amezipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kusikiliza na kushughulikia masuala ya wafanyakazi, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha majadiliano kati ya Serikali na wafanyakazi ili kupata ufumbuzi endelevu wa changamoto zinazojitokeza.
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...