Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndugu Abdi Mahamoud Abdi, amempongeza Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Ndugu Faris Burhan, kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo, huku akimtaka kuendeleza juhudi za kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa vijana.
Abdi ameyasema hayo alipompokea Faris aliyewasili katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar, ambapo amewahimiza vijana kutumia fursa za maendeleo zinazotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujikwamua kiuchumi na kuchangia maendeleo endelevu ya nchi.
Kwa upande wake, Faris ameishukuru CCM Zanzibar kwa mapokezi aliyoyapata, akieleza kuwa yanaakisi umoja na mshikamano miongoni mwa vijana wa chama hicho.
Aidha, amewapongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa kuwaamini vijana na kuwapa nafasi za uongozi ndani ya Chama na Serikali.
Amesema ataendelea kusimamia UVCCM katika kutekeleza maono ya viongozi wa CCM, kwa kuimarisha umoja na mshikamano, kujenga imani miongoni mwa wanachama na vijana, pamoja na kuendeleza misingi na maadili ya chama hicho.
Baada ya kuwasili Kisiwandui, Faris alitembelea kaburi la Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, na kumuombea dua.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...