Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Richard Kasesela, ameshiriki mazishi ya aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, marehemu Said Goha, yaliyofanyika katika Kata ya Mtimbila, Wilaya ya Malinyi, Mkoa wa Morogoro, aliyefariki dunia hivi karibuni katika ajali ya barabarani.
Akizungumza akiwa msibani, Kasesela amesema marehemu Goha alikuwa mzalendo na mwanamapinduzi wa kweli aliyekuwa na msimamo thabiti katika kukitetea chama chake, akisisitiza kuwa hakupenda kuona CCM ikishindwa wala mtu yeyote akionewa.
Amesema msimamo huo unaonesha namna marehemu alivyokuwa akisimamia misingi ya haki, usawa na maslahi ya chama pamoja na watu aliowatumikia.
Kasesela amesema mchango wa marehemu Goha katika kukijenga na kukiimarisha chama hautasahaulika, huku akitoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wanachama wa CCM kutokana na msiba huo, akiwataka kuendelea kuthamini mema aliyoyaacha marehemu katika maisha yake na utumishi wake kwa chama na jamii.

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...