Na Farida Mangube
Matokeo ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Cardiff nchini Uingereza yameonesha umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa visima binafsi, uvunaji wa maji ya mvua na matumizi ya teknolojia za kurejeleza maji yaliyotumika, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dodoma.
Matokeo hayo yamewasilishwa katika Warsha ya Kuwasilisha na Kuhakiki Matokeo ya Utafiti wa Mradi wa Water Resilient Cities iliyofanyika jijini Dodoma, ambapo Kiongozi wa Mradi kutoka Tanzania, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utafiti na Shahada za Uzamili SUA, Prof. Japhet Kashaigili, amesema utafiti huo ulioanza mwaka 2022 umelenga kubaini changamoto za upatikanaji wa maji na namna bora ya kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi wote kwa usawa na kwa njia endelevu.
Prof. Kashaigili amesema licha ya jitihada za Serikali kuongeza vyanzo vya maji, mahitaji katika Jiji la Dodoma bado ni makubwa kuliko kiwango kinachozalishwa, hali inayosababisha wananchi wengi kutegemea visima binafsi.

Ameeleza kuwa uchimbaji wa visima bila uratibu wa kutosha unaweza kuathiri upatikanaji wa maji katika visima vingine vilivyo karibu na kusababisha migogoro baina ya wananchi, hivyo amesisitiza umuhimu wa kufuata taratibu za kisheria za uchimbaji wa visima.
Aidha, Prof. Kashaigili amesema matokeo ya utafiti huo, unaohusisha pia miji ya Cape Town nchini Afrika Kusini, Windhoek nchini Namibia na Lagos nchini Nigeria, yatasaidia kuboresha mipango ya usimamizi wa rasilimali za maji, ikiwemo kuanzisha mifumo ya kurejeleza maji yaliyotumika katika shughuli zisizohitaji maji ya kunywa.
Kwa upande wake, Juliana Sankel kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Wilaya ya Dodoma, akitoa mtazamo wake baada ya kupokea matokeo ya utafiti huo, amesema yatasaidia kubaini vyanzo mbadala vya maji na kuboresha mipango ya usambazaji wa huduma hiyo badala ya kuendelea kutegemea maji ya chini ya ardhi pekee.
Naye Mtaalamu wa Utafiti wa Maji Chini ya Ardhi na aliyewahi kufanya kazi katika Ofisi ya Bonde la Wami-Ruvu, Catherine Mwihumbo, amesema matokeo hayo yatasaidia kuimarisha usimamizi wa vyanzo vya maji na uhifadhi wa mazingira.

Amependekeza kuhamasishwa kwa uvunaji wa maji ya mvua, ujenzi wa mabwawa na uandaaji wa ramani za maeneo yenye maji chini ya ardhi ili kudhibiti uchimbaji holela wa visima na kuongeza upatikanaji endelevu wa maji katika Jiji la Dodoma.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...