Na Vero Ignatus, Michuzi TV – Arusha
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imesisitiza umuhimu wa mabadiliko ya kidijitali katika sekta ya posta na usafirishaji wa mizigo ili kurahisisha biashara za mipakani, kuongeza ufanisi wa huduma na kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kufikia masoko mapana.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Sweetbert Zakaria Mkama, wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Tano la Mawasiliano, Posta na Usafirishaji Afrika Mashariki lililofanyika jijini Arusha, ambapo amehimiza nchi wanachama kuacha mijadala na kuelekea katika utekelezaji wa suluhisho za kiteknolojia.
Amesema matumizi ya akili unde (AI), uchambuzi wa takwimu na mifumo ya kufuatilia mizigo kwa wakati halisi yanaweza kuboresha huduma za posta na usafirishaji, huku ushirikiano wa kikanda ukiwa muhimu katika kurahisisha biashara na mifumo ya malipo baina ya nchi wanachama.
Kwa upande wake, mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Dk. Peter Kihogo, amesema hadi Juni 2026, mtandao wa mawasiliano ya simu wa kizazi cha nne (4G) ulikuwa umefikia asilimia 94 ya wananchi. Aidha, mfuko huo umesambaza vifaa vya kidijitali zaidi ya 500, kompyuta 100 na mashine 50 za kunakili nyaraka kwa ajili ya kuboresha huduma za posta.
Ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2026/2027, UCSAF imepanga kujenga majengo 31 ya posta vijijini ili kuongeza upatikanaji wa huduma hizo, hususan kwa wananchi wa maeneo ambayo hayajafikiwa vya kutosha na miundombinu ya mawasiliano na usafirishaji.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, amesema Arusha imependekezwa kuwa eneo la majaribio la kuanzisha na kuimarisha huduma za posta za kidijitali. Mpango huo unalenga kuzifanya ofisi za posta kuwa vituo vya kisasa vinavyounganisha wananchi na biashara mtandaoni, malipo ya kidijitali na huduma za serikali mtandao.
Katika jukwaa hilo, Shirika la Posta Tanzania limewasilisha mfumo wa Posta Kiganjani, unaopatikana kupitia simu za mkononi na tovuti, unaowawezesha wananchi kupata huduma za kifedha, biashara mtandaoni na usafirishaji wa bidhaa bila kulazimika kutembelea ofisi za posta kwa kila huduma.
Wadau walioshiriki jukwaani hapo, wakiwemo Caroline Kanuti na Michael Njao, wameeleza umuhimu wa kuoanisha mifumo ya teknolojia, malipo na usafirishaji katika nchi za Afrika Mashariki. Hatua hiyo inalenga kupunguza vikwazo vya biashara za mipakani, kuongeza ufanisi wa huduma za posta na kufungua fursa zaidi za kiuchumi kwa wananchi na wafanyabiashara katika ukanda huo.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...