Na Janeth Raphael -MichuziTv
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amefafanua kuwa makadirio ya Shilingi Bilioni 730 yaliyotajwa katika Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kujiandaa na Kukabiliana na Madhara ya El Niño kwa mwaka wa fedha 2026/2027 si bajeti mpya ya Serikali, bali ni jumla ya makadirio ya rasilimali zinazohitajika kutoka taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali kwa ajili ya kutekeleza shughuli za kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Oktoba 25, 2026, Msigwa amesema mpango huo umeandaliwa kufuatia utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ulioonesha uwezekano wa kutokea kwa El Niño yenye nguvu na kusababisha madhara yakiwemo mafuriko, maporomoko ya ardhi na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama.
Amesema maandalizi ya mpango huo yaliratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikisha Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa, mashirika ya kitaifa na kimataifa, taasisi zisizo za kiserikali pamoja na sekta binafsi. Amefafanua kuwa taasisi hizo zitatekeleza majukumu yake kwa kutumia rasilimali na bajeti zilizoidhinishwa kwa mwaka wa fedha 2026/2027, huku kipaumbele kikitolewa kwa shughuli za kulinda maisha na mali za wananchi.
Kwa mujibu wa Msigwa, shughuli zilizopangwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara, madaraja na mitaro, kuimarisha huduma za afya, elimu, maji na umeme, kuhifadhi akiba ya chakula, kununua vifaa vya uokoaji, kuandaa maghala ya misaada ya kibinadamu na makazi ya muda kwa wananchi watakaolazimika kuhama maeneo hatarishi. Serikali pia itaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na majanga.
Katika hatua nyingine, Msigwa amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoanzishwa, akieleza kuwa utekelezaji wake unaendelea katika hatua tofauti kulingana na upatikanaji wa rasilimali. Amesema pamoja na dhamira ya kukamilisha miradi yote, Serikali haiwezi kutekeleza mahitaji yote kwa wakati mmoja, hivyo baadhi ya miradi hutekelezwa kwa awamu ili kuzingatia vipaumbele vya maendeleo na majukumu mengine ya kitaifa.
Akizungumzia maendeleo yaliyofikiwa, Msigwa amesema idadi ya watu nchini imeongezeka kutoka milioni 12.3 mwaka 1967 hadi takribani milioni 70 mwaka 2026, huku umaskini wa mahitaji ya msingi ukipungua kutoka asilimia 38.6 mwaka 1991/92 hadi asilimia 25.1 mwaka 2025. Aidha, ametoa wito kwa wananchi kufuatilia taarifa rasmi za tahadhari zinazotolewa na TMA na mamlaka husika, huku akizitaka pia taasisi za habari kuzingatia weledi, maadili na misingi ya uandishi wa habari katika kuripoti masuala ya umma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...