Na Said Mwishehe,Michuzi TV

VYAMA vya Akiba na Mikopo(SACCOS) nchini Tanzania vimefanikiwa kujiimarisha kiuchumi kwa kuwa na mtaji unaozidi Sh.Trilioni 1.7 ambao unaweza kusaidia kuchochea ukuaji wa uchumi iwapo utaelekezwa katika shughuli za uzalishaji.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kongamano la 26 la Kimataifa la Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo Barani Afrika (SACCA).Kongamano hilo linaendelea jijini Dar es Salaam.

“Uwepo wa fedha hizo katika SACCOS ni fursa ya kuimarisha sekta za uzalishaji zinazohitaji mitaji nafuu ili kuongeza uzalishaji, kupanua biashara na kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi,”amesema Mweli.

Pia amsema kupitia kongamano hilo moja ya malengo ya majadiliano hayo ni kuhakikisha fedha zinazokusanywa na SACCOS zinawekezwa katika sekta za uzalishaji zinazohitaji mikopo yenye riba nafuu, badala ya kubaki bila kutumika ipasavyo katika kuchochea shughuli za kiuchumi.

Amesisitiza kwamba Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika, kwa kushirikiana na jumuiya ya vyama vya ushirika vya akiba na mikopo nchini, inaendelea kuimarisha ushirikiano kati ya SACCOS na vyama vingine vya ushirika ambavyo vinajihusisha na shughuli za uzalishaji.

“Hatua hii itasaidia kuunganisha vyama vya akiba na mikopo na vyama vya wakulima, wafugaji na vyama vingine vya uzalishaji ili kurahisisha upatikanaji wa mitaji na kukuza masoko ya bidhaa zao.

Kuhusu kongamano hilo ambalo limeshirikisha washiriki zaid ya 600 kutoka katika mataifa 28 barani Afrika Mweli amesema limetoa nafasi ya kubadilishana uzoefu na kuimarisha mitandao ya mawasiliano kati ya SACCOS za Tanzania na nchi nyingine za Afrika.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...