KAMPUNI ya Meridianbet imeendeleza dhamira yake ya kuwa sehemu ya mabadiliko chanya katika jamii kwa kutoa msaada wa vifaa vya usafi katika Hospitali ya Kambangwa, iliyopo Mwananyamala, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Msaada huo ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo za kuhakikisha inagusa maisha ya wananchi kupitia programu zake za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

Kupitia hatua hiyo, Meridianbet imeonyesha kuwa mchango wa kampuni katika jamii haupimwi kwa shughuli za kibiashara pekee, bali pia kwa namna inavyoshiriki kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kusaidia taasisi zinazotoa huduma muhimu kwa umma.

Makabidhiano hayo yamefanyika kwa ushirikiano baina ya Meridianbet na uongozi wa Hospitali ya Kambangwa, huku yakilenga kuimarisha mazingira ya usafi ndani na nje ya hospitali hiyo. Jitihada hizo zinatarajiwa kusaidia kuboresha mazingira ambayo ni sehemu muhimu ya utoaji wa huduma bora za afya.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na buti (Boots), mifagio mikubwa ya kusafishia sakafu (Big Mop), mapipa ya taka (Dustbins) pamoja na sabuni maalumu ya kuua vijidudu (Disinfectant Soap), ambavyo vitatumika kurahisisha shughuli za usafi na utunzaji wa mazingira yanayoizunguka hospitali.

Akizungumza katika tukio hilo, Nancy Ingram kutoka Meridianbet amesisitiza kuwa kuisaidia jamii yenye uhitaji ni sehemu ya msingi wa shughuli za kampuni hiyo, akieleza dhamira ya Meridianbet kuendelea kushiriki katika mipango yenye manufaa kwa wananchi.

"Kusaidia jamii zenye uhitaji ni miongoni mwa misingi muhimu ya kampuni yetu. Tunaamini kila mchango unaolenga kutatua changamoto za wananchi unaweza kuwa na nafasi kubwa katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii," amesema Nancy Ingram.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

 

Meridianbet inaendelea kutumia programu zake za CSR kama nyenzo ya kuimarisha ushirikiano na taasisi mbalimbali, kwa kutambua kuwa maendeleo ya jamii yanahitaji ushiriki wa wadau wote. Kupitia msaada huo, kampuni inaendeleza ujumbe wake kwamba kujali jamii si kauli pekee, bali ni dhamira inayopaswa kuonekana kupitia matendo yanayoboresha maisha ya watu.

 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...