Na Victor Masangu, Pwani
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mlezi mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, amewataka viongozi wa chama hicho kuachana na vitendo vya kuunda makundi, magomvi na mivutano, akisema hali hiyo inaweza kudhoofisha umoja na misingi ya chama.
Akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Pwani katika Ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, eneo la Kwa Mfipa, Kibaha, amesema amekuja kukilea chama kwa ujumla na si makundi ndani ya chama.
"Chama chetu ni chama kilicho madarakani na kinapendwa sana na wananchi, lakini hakiwezi kujengwa kwa makundi wala mivutano," amesema Abdulla.
Amesisitiza kuwa viongozi wote wanapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano na mshikamano, huku wakizingatia Katiba, Kanuni na miongozo ya CCM katika kusimamia shughuli za chama.
Ameongeza kuwa hakuna sababu ya viongozi kuvutana, akieleza kuwa migogoro na mivutano ni kama sumu inayoweza kukiumiza chama.
Katika hatua nyingine, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kile alichokieleza kuwa ni kurejesha heshima ya CCM na kuimarisha hali ya amani na utulivu nchini.
Kwa upande wao, baadhi ya viongozi wa CCM Mkoa wa Pwani wameahidi kumpa ushirikiano Mlezi huyo mpya na kutekeleza maelekezo aliyoyatoa kwa lengo la kuimarisha umoja na uendeshaji wa chama mkoani humo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...