WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amewataka wajasiriamali nchini na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuongeza ubunifu, ubora na ushindani wa bidhaa zao ili kunufaika na fursa za masoko zinazotokana na ushirikiano wa kikanda.

Sangu ametoa wito huo Novemba 6, 2026, jijini Kigali, Rwanda, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Tanzania katika Maonesho ya 26 ya Jua Kali yanayofanyika nchini humo.

Amesema ubunifu ni nyenzo muhimu katika kukuza biashara na kuongeza ushindani wa bidhaa katika masoko ya ndani na kimataifa, huku akiwapongeza wajasiriamali wa Tanzania kwa kazi zao bunifu.

Amesema maonesho hayo ni jukwaa muhimu la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kupanua masoko, kukuza biashara na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi wa nchi wanachama wa EAC.

Ameongeza kuwa maonesho hayo yamefanyika kwa mara ya 26 tangu kuanzishwa mwaka 1999 jijini Arusha, Tanzania, na mwaka huu yanashirikisha zaidi ya wajasiriamali 2,500 kutoka nchi wanachama, ikilinganishwa na 2,241 mwaka jana.

Aidha, ametaja changamoto zinazokabili sekta hiyo kuwa ni pamoja na upatikanaji wa mitaji, maeneo ya biashara, masoko, elimu ya ujasiriamali na viwango vya ubora wa bidhaa, pamoja na mazingira yasiyo bora ya kufanyia kazi, akiahidi kuzifanyia kazi kupitia nchi wanachama.

Maadhimisho ya Siku ya Tanzania yamepambwa na maonesho ya mavazi ya asili, ambapo wajasiriamali wameonesha bidhaa mbalimbali zikiwemo mavazi ya Kitenge na Batiki, mikoba na viatu vya ngozi pamoja na vyakula vya asili vya jamii za Tanzania.a







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...