BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imetoa Tuzo za Umahiri katika Uandaaji wa Taarifa za Fedha (Best Presented Financial Statements Awards), kwa kutambua na kuzipongeza taasisi zilizofanya vizuri katika uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za fedha.
Tuzo hizo zimetolewa katika hafla iliyofanyika Novemba 26, 2026, katika viwanja vya APC, Bunju, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya shughuli za Mkutano Mkuu wa 39 wa Mwaka wa Wahasibu.
Kupitia tuzo hizo, NBAA inalenga kuhamasisha Taasisi za umma na binafsi kuzingatia viwango vya kitaaluma katika uandaaji wa taarifa za fedha, huku ikikuza uwazi, uwajibikaji na uaminifu katika usimamizi wa fedha.
Tuzo hizo pia zinatambua juhudi za Taasisi zinazozingatia viwango vya Uhasibu na matakwa ya uandaaji wa taarifa za fedha, pamoja na kuhamasisha Taasisi nyingine kuimarisha mifumo yao ya usimamizi na utoaji wa taarifa za fedha.
Hafla hiyo imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya Uhasibu na fedha, ambao wamepata fursa ya kutambua mafanikio ya Taasisi zilizofanya vizuri katika uandaaji wa taarifa za fedha.
Washindi wa tuzo hizo wamepatikana katika makundi mbalimbali ya Taasisi, zikiwemo kampuni, mashirika na Taasisi za umma na binafsi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nsubili Joshua akisoma hotuba ya utoaji wa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2025 (Best Presented Financial Statements for the Year 2025 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia S. Temu akizungumza kuhusu hatua zilizofanyika mpaka upatikanaji wa washindi hao wakati wa utoaji wa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2025 (Best Presented Financial Statements for the Year 2025 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA)Mkurugenzi wa Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Siasa Mzenzi akitoa neno wakati wa utoaji wa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2025 (Best Presented Financial Statements for the Year 2025 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa mgeni rasmi pamoja na wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika Hotel ya APC Bunju Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nsubili Joshua akikabidhi tuzo kwa Viongozi mbalimbali wa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika yaliyofanya vizuri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2025 (Best Presented Financial Statements for the Year 2025 Awards) zinayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA)Baadhi ya wadau waliofika kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2025 (Best Presented Financial Statements for the Year 2025 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) zilizofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Washindi mbalimbali wa Tuzo zilizotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa utoaji wa tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2025 (Best Presented Financial Statements for the Year 2025 Awards) kwa Taasisi, Makampuni pamoja na Mashirika zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwenye hafla iliyofanyika katika Hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nsubili Joshua akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) wakati wa utoaji wa tuzo za umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2025 (Best Presented Financial Statements for the Year 2025 Awards) kwenye hafla iliyofanyika katika Hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.



































Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...