Meya wa Jiji la Mwana na Mwenyekiti mpya ALAT Taifa, akipokea zawadi kutoka kwa Meneja PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki, CPA Rajabu Kinande alipotembelea huduma za PSSSF zinazoendelea kutolewa katika maonyesho yanayofanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa 40 ALAT
Mhe. Isack Joseph Copriano, Mbunge wa Monduli (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa PSSSF mara baada ya kutembelea banda la PSSSF katika maonyesho yanayofanyika sambamba na kikao cha 40 cha Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT)
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unashiriki katika maonesho yanayoambatana na Mkutano Mkuu wa 40 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), yanayofanyika jijini Mwanza.
Mkutano huo umefunguliwa rasmi Novemba 16, 2026, na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, na unatarajiwa kuhitimishwa Novemba 20, 2026.
Akizungumzia ushiriki wa Mfuko katika maonesho hayo, Meneja wa Kanda ya Ziwa Mashariki wa PSSSF, CPA Rajab Kinande, amesema mkutano huo ni fursa muhimu kwa Mfuko kukutana na wadau wake, hususan watumishi wa Serikali za Mitaa, ambao ni miongoni mwa wanachama wake.
Amesema kupitia maonesho hayo, watumishi hao watapata fursa ya kufahamu majukumu ya Mfuko, huduma zinazotolewa pamoja na maboresho mbalimbali yaliyofanyika kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wanachama na wastaafu na hatimaye kufikia lengo kama kauli mbiu isemavyo ‘tunalipa jana’
Aidha, amesema ushiriki wa PSSSF katika maonesho hayo ni sehemu ya jitihada za Mfuko za kusogeza huduma karibu na wanachama wake, kuwaelimisha kuhusu haki na stahiki zao pamoja na kuwajengea uelewa wa namna bora ya kutumia mifumo ya kidijitali inayowezesha upatikanaji wa huduma kwa urahisi na haraka.







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...