Na Mwandishi Wetu, Dar.
Kampuni ya Tiba Healthcare imefanya matembezi ya kupambana na Kisukari (Diabetes) 'TIBA TWENDE' katika kuadhimisha Wiki ya Magonjwa Yasiyoambukiza inayofanyika wiki ya pili ya Novemba kila mwaka.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Projesh Mtasingwa, ameitaka jamii kufanya mazoezi, kula mlo kamili na kupima afya mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza, ikiwemo kisukari.
Amesema kampeni ya mwaka huu ni chini ya kauli mbiu, "Zijue Namba Zako, Chukua Hatua, Okoa Maisha," na kwamba watu wengi huishi na magonjwa hayo bila kujua hadi matatizo yanapotokea, hivyo vipimo vya mara kwa mara ni muhimu.
Ametaja kutofanya mazoezi, ulaji mbaya, pombe kupita kiasi na tumbaku kama sababu kuu za hatari. Amewashauri wananchi kufanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku, siku tano kwa wiki, kula matunda na mboga za majani, kupunguza chumvi, sukari, pombe na tumbaku, na kupata usingizi wa kutosha.
Ametaja kisukari, saratani, magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, magonjwa sugu ya upumuaji na matatizo ya afya ya akili kama magonjwa ya kawaida yasiyoambukiza, ambayo udhibiti wake unahitaji serikali, sekta binafsi na jamii.
Mratibu wa Magonjwa Yasiyoambukiza wa Mkoa, Dkt. Livin Nyaki, amesema magonjwa hayo yanachangia takriban asilimia 40 ya vifo nchini, kutokana kwa sehemu na mitindo ya maisha ya kukaa bila shughuli. Amewasihi wananchi kupima afya mara kwa mara hata bila dalili, kwani utambuzi wa mapema huongeza fursa za matibabu. Ameipongeza Tiba Health Care kwa kushirikiana na mamlaka kuhimiza kinga.
Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Tiba Health Care, Arun Sharma (COO), amesema matembezi hayo yanalenga kupinga dhana kuwa kisukari huathiri wazee pekee, kwani vijana pia wako hatarini kama hawatachukua hatua za haraka.
Daktari wa Tiba Healthcare, Dkt. Sabreen Dihalla Bamdali, amesema matembezi hayo yamelenga kuongeza uelewa kuhusu kisukari, akibainisha kuwa THCL wamekuwa wakitoa huduma hiyo kwa watu mbalimbali. Amesisitiza jamii kujenga utamaduni wa mazoezi na lishe bora.
Washiriki akiwemo Mohamed Ali kutoka Unity Cycling Group, wamehimiza mazoezi kuwa sehemu ya maisha ya kila siku, wakisema matembezi, kukimbia na kuendesha baiskeli ni njia rahisi za kuimarisha afya.
Tiba Healthcare Ltd ni kituo binafsi cha afya (Specialized Polyclinic) kilichopo Mtaa wa Magore, Upanga Mashariki, kinachotoa huduma za dawa za ndani, upasuaji, mifupa, macho, meno, na magonjwa ya moyo.
Matembezi ya Tiba Twende mwaka huu ni msimu wa kwanza, na yanatarajia kuwa endelevu kila mwaka.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...