-Pia yaweka mkakati kuimarisha mtandao wa simu katika SGR Dar -Dodoma


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

SERIKKALI kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF) inatekeleza mradi wa kutoa huduma za bure za intaneti kwenye maeneo ya wazi ili wananchi kuweza kutumia huduma ya intaneti bure katika maeneo hayo muhimu ambayo yanawatumiaji wengi.

Hayo yamesemwa leo Novemba 3,2026 jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa UCSAF Albart Richard alipokuwa akizungumza katika kikao kazi kilichohusisha Wahariri wa vyombo vya habari na waandishi chini ya uratibu wa ofisi yq Msajili wa Hazina.

Amesema kupitia mradi huo, vituo vya Intaneti 17 vimeanzishwa katika Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba, Dar es Salaam.

Vilevile, vituo vya intaneti vimeanzishwa katika maeneo ya viwanja vya Nyerere Square (Dodoma), College of Informatics CIVE (Dodoma), Soko la Nyamagana (Mwanza), Kiembesamaki (Zanzibar), Soko la Tabora (Tabora), Lungemba Training college in Mafinga.

“Huduma ya kutoa huduma bure za Intaneti bure katika maeneo ya wazi.Changamoto iliyopo tunapokamilisha mradi huo tunapowakabidhi wahusika wanashindwa kumudu zile gharama za kutoa huduma hiyo bure.

“Tunapotekeleza mradi huwa kwa muda fulani kwa mfano mwaka mmoja au miaka miwili UCSAF huwa tunalipia gharama ,sasa tunapokabidhi kwa halmashauri husika wanashindwa kumudu gharama maana tunaposema tunatoa huduma za intanet bure maana yake mfuko wetu unalipia.

“Hivyo tunafikiria njia nzuri itakayowezesha kutatua changamoto hiyo,kwa mfano Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) wao wanayo huduma hiyo ingawa mtumiaji anapotumia huduma hiyo baada ya robo saa au nusu saa anatakiwa kulipia.”

Wakati huo huo amesema UCSAF imepanga kutekeleza mradi wa kuimarisha mawasiliano ya simu katika maeneo ya kimkakati yakiwemo ya Reli ya Kisasa ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.

“Katika Mradi wa Awamu ya 11 Serikall kupitia UCSAF, imepanga kutekeleza mradi wa kukamilisha mawasilano ya simu ketika maeneo

ya kımkakali ya SGR,MGR, reli ya TAZARA,maeneo ya mipakani na Hifadhi za Taifa.”

Akizungumzia miradi ya TEHAMA katika sekta ya elimu, amesema shule za umma 1,167 zimenufaika na mradi wa kupeleka vifaa vya TEHAMA na kujenga maabara, huku Serikali ikiwa imewekeza Sh17.7 bilioni hadi Oktoba 2026 katika utekelezaji wake.

Ameongeza UCSAF imepeleka vifaa maalumu vya TEHAMA katika shule 22 zinazohudumia wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Vifaa hivyo ni pamoja na mashine za nukta nundu,kompyuta maalumu, vifaa vya kurekodi sauti na vifaa vya kukuza maandishi, kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi hao kupata elimu kwa usawa.

Kuhusu kuwajengea uwezo watumiaji wa teknolojia, Mhandisi Richard amesema walimu 5,094 wa shule za msingi na sekondari za umma Tanzania Bara na Zanzibar wamenufaika na mafunzo ya TEHAMA tangu mwaka wa fedha 2016/2017.“Pia wanafunzi wa kike 1,581 wamejengewa uwezo kupitia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika TEHAMA.”



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...