MKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela, Agosti 24, 2026 amepokea rasmi Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Shinyanga.
Hafla ya mapokezi imefanyika katika Kijiji cha Nyang'holongo, Kata ya Nundu, Wilaya ya Nyang'hwale.
Akizungumza baada ya kupokea mwenge huo, Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa wa Geita kwa mwaka 2026 utakimbizwa katika Halmashauri 6.
Atanzia na Halmashauri ya Nyang'hwale hadi kumalizia katika Halmashauri ya Chato, kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa.
Ameeleza kuwa wakati wa ukimbizaji wa Mwenge Mkoani Geita, utakimbizwa kwa umbali wa Kilometa 698.2.
Katika kipindi hicho jumla ya miradi 42 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 168.74 itapitiwa. Miradi hiyo itazinduliwa, kuekwa mawe ya msingi, kukaguliwa na kutembelewa.
CRDB Bank imeshiriki katika kilele cha Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026, kinachofanyika Jijini Tanga, ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa wadau mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi katika maadhimisho hayo.
Ushiriki wa CRDB Bank unaendelea kuakisi nafasi ya sekta ya fedha katika kuchangia jitihada zinazolenga kuimarisha elimu, ujuzi na ubunifu kama nyenzo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini
John Mtani, Meneja Mwandamizi wa Biashara za Serikali, CRDB Bank, akishiriki katika kilele cha Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026 jijini Tanga, pamoja watumishi, viongozi mbalimbali na wananchi waliotembelea Banda la CRDB Benki.Akizungumza katika kikao cha Baraza la wazee cha robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Sumbawanga Herry Sanga amesema wamefanikiwa kutoa vitambulisho vya msamaha wa matibabu ikiwa wanawake 138, wanaume 108 huku wazee 29 ambao hawakuwa na vitambulisho vya msamaha wa matibabu wamepewa msamaha wa muda wa matibabu.
Kwa upande wake katibu wa Baraza la wazee Manispaa ya Sumbawanga Moris Massanja amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa wazee kuhusu haki zao pamoja na huduma zinazopatikana kwa ajili yao.
Utoaji wa vitambulisho vya msamaha wa matibabu kwa wazee unalenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na kuhakikisha wazee wanapata huduma za matibabu kwa wakati na bila vikwazo vinavyotokana na ukosefu wa vitambulisho.
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili leo Jumatatu, Agosti 24, 2026, katika Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Tanga, ambapo anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, mkoani Tanga.
Amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Batilda Burian, pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda.
Alipowasili katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, Waziri Mkuu ametembelea mabanda mbalimbali ya maonesho na kujionea bunifu, teknolojia na kazi mbalimbali zinazowasilishwa na washiriki katika maadhimisho hayo.

Wito huo umetolewa na Diwani wa Kata ya Kwembe katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Kawina Hadji Konde, alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya saba ya Shule ya Awali na Msingi ya Mwendo, iliyopo Kibamba kwa Mangi, wilayani Ubungo.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyowakutanisha wazazi, walimu, wanafunzi na wadau mbalimbali wa elimu, Bw. Konde alisema shule binafsi na zile za Serikali zina nafasi kubwa ya kujenga mifumo ya ushirikiano katika maeneo mbalimbali, ikiwemo elimu, michezo, sanaa, utamaduni na shughuli za kijamii, kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kuinua viwango vya elimu kwa manufaa ya wanafunzi na jamii kwa ujumla.
Alisema ushindani kati ya shule unapaswa kujengwa katika misingi chanya inayochochea ubunifu, ubora wa ufundishaji na ujifunzaji, badala ya kuwa kikwazo cha ushirikiano kati ya taasisi hizo.
“Kwenye hili niwapongeze sana uongozi wa Shule ya Mwendo kupitia Mkuu wa Shule, Mwalimu Adolf Nyabarimba, ambaye kwa kweli amekuwa mdau mkubwa na mzuri katika masuala mbalimbali yanayohusu Kata yetu ya Kwembe. Amekuwa akishiriki vikao na mikutano mbalimbali inayohusiana na kata yetu kila anapohitajika na amekuwa akitoa ushirikiano wakati wote. Huu ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wa shule nyingine, kwa sababu shule ni sehemu ya jamii,” alisema Bw. Konde.
Aidha, Bw. Konde aliwasisitiza wazazi kuongeza ushirikiano na walimu katika malezi ya watoto, akieleza kuwa elimu bora haiishii darasani pekee, bali inahitaji pia misingi imara ya maadili, uwajibikaji, uzalendo na malezi yenye mwelekeo chanya.
Aliwataka wazazi na walezi kuwa karibu zaidi na watoto wao, kuwafuatilia na kuwasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii zinazoweza kuathiri ustawi wao wa kimwili na kisaikolojia, huku akisisitiza umuhimu wa kujenga mazingira salama kwa watoto ndani na nje ya shule.
Kwa upande wake, uongozi wa Shule ya Mwendo ulieleza umuhimu wa ushirikiano kati ya shule, wazazi na jamii katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu inayowaandaa kuwa raia wenye maarifa, nidhamu, ubunifu na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.
Mahafali hayo yalipambwa na burudani na maonesho mbalimbali yaliyoandaliwa na wanafunzi, yakiwemo muziki, sanaa, utamaduni, ukakamavu pamoja na maonesho ya kitaaluma, yaliyowapa wazazi na wageni fursa ya kushuhudia vipaji na uwezo wa wanafunzi nje ya masomo ya darasani.
Diwani wa Kata ya Kwembe, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Kawina Hadji Konde (wa pili kulia), akimkabidhi Manal Salum, mwanafunzi wa darasa la saba, zawadi ya Mwanafunzi Bora wa Kike katika Shule ya Awali na Msingi ya Mwendo, iliyopo Kibamba kwa Mangi, Wilaya ya Ubungo, wakati wa hafla ya mahafali ya saba ya shule hiyo, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia tukio hilo ni viongozi na walimu wa shule hiyo.
Diwani wa Kata ya Kwembe, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Kawina Hadji Konde (wa tatu kulia), akimkabidhi Olivia Kassim, mwanafunzi wa elimu ya awali, cheti cha kuhitimu elimu hiyo katika Shule ya Awali na Msingi ya Mwendo, iliyopo Kibamba kwa Mangi, Wilaya ya Ubungo, wakati wa hafla ya mahafali ya saba ya shule hiyo, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia tukio hilo ni viongozi na walimu wa shule hiyo.
Mahafali hayo yalipambwa na burudani na maonesho mbalimbali yaliyoandaliwa na wanafunzi, yakiwemo muziki, sanaa, utamaduni, ukakamavu pamoja na maonesho ya kitaaluma, yaliyowapa wazazi na wageni fursa ya kushuhudia vipaji na uwezo wa wanafunzi nje ya masomo ya darasani.
Katika mahafali hayo, walimu, wazazi na wanafunzi walipata wasaa wa kucheza pamoja ili kujipongeza kwa hatua hiyo muhimu.

















.jpeg)


.jpeg)


.jpeg)









.jpeg)
.jpeg)



.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)







