Home
Unlabelled
jero
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Kaka
ReplyDeleteMimi nafikiri, kwa vile walikuwa wanaenzi chuo Kikuu, cha Dar es salaam kwenye Jero,Huyo nyoka anawakilisha tiba, ambacho ni uwakilishi wa chuo kikuu kishiriki cha Muhimbili. Chunguza letter head za Muhimbili utagundua kuwa kuna nyoka. Wenyewe wanamwita nyoka wa utabibu.
huyo nyoka anawakilisha rushwa, hilo jengo hapo ni benki kuu(hela). huwezi kuingia ndani yajengo(kupata hela) bila kumfurahisha nyoka(kutoa/kula rushwa)
ReplyDeletehiyo ndo bongo
That's a Caduceeus, and has often used through out the centuries to represent health. In the states and other nations they use two snakes instead.
ReplyDeleteThe symbol's origins are thought to date to as early as 2600 BC in Mesopotamia, and there are several references to a caduceus-like symbol in the Bible, namely in Numbers 21:49, and 2 Kings 18:4. During the Exodus, Moses was instructed by God to fashion a pole upon which he was to position a serpent made of bronze; when looked upon, this Nehushtan, as it was called in Hebrew, would spare the lives of the Israelites stricken by venomous snake bites.
The intent was that people would look upward and be reminded to pray to God, but eventually the meaning was forgotten and this symbol was apparently worshiped by the Hebrew people until the reign of Hezekiah as described in 2 Kings 18:4.Walter Burkert has two figures in his book which show a rod with two intertwined snakes winding around a central axis from Mesopotamia in 2200 BC, and a similar image from Crete in 700 BC.
That's just a glimpse of the symbols history. Over the years it got adopted and transformed by different civilizations (e.g the Romans)
For a more detailed history you can check out this link.
http://www.crystalinks.com/caduceus.html
~Dave
Ninajaribu kujibu swali la mwanakijiji mwenzetu alyeuliza maana ya alama ya nyoka iliyo katika noti. Sifahamu ni kwa nini serikali iliweka alama ila ninajua kuwa alama hiyo ina maana ya kiutabibu. Maana ya alama hiyo kiutabibu inatokana na simulizi lililomo katika Biblia kitabu cha Hesabu sura ya 21. Katika simulizi hilo inaonyeshwa kuwa baada ya Waisraeli kuondolewa utumwani Misri walimnung'unikia Mungu kuwa amewapeleka jangwani kusiko na chakula wala maji. Kwa sababu ya manung'uniko hayo, Mungu "aliwatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa" (Hes. 21:6). Baada ya kuona haya, watu wakamwendea Musa kiongozi wao na kusema, "Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu." Wakamwomba Musa awaombee kwa Mungu ili awasamehe na awaondolee wale nyoka. Musa alipomwomba Mungu kwa niaba ya watu wake, Mungu alimwambia Musa, "Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, na akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi" (Hes. 21:8-9).
ReplyDeleteKutokana na historia hii, mashirika mengi yanayohusika na mambo ya tiba yanatumia nembo hii ya nyoka aliyening'inizwa kwenye mti kama alama ya tiba.
Kwa Wakristo, kifo cha Yesu msalabani kinabeba ishara ya nyoka aliyening'inizwa mtini. Ndiyo maana upo mkazo kuwa Yesu ni tiba ya magonjwa yote, ikiwa ni pamoja na gonjwa la dhambi. Mtu akimtazama yetu atapona, naam, ataishi.
Sina hakika kama maana niliyoieleza hapa ndiyo maana iliyokusudiwa na walioiweka picha ya nyoka aliyening'inizwa kwenye mti katika noti. Inawezekana wana maana hiyo hiyo.
Bro Michuzi
ReplyDeleteHy pengine ni alama ya afya!
anawakilisha madawa ya asili tuliyojaaliwa na mola
ReplyDeleteInawakilisha chuo kikuu upande wa Muhimbil.
ReplyDeleteMichuzi, hiyo noti upande huo umewekwa rasmi kwa ajili ya wanataaluma wa nchi yetu. Ukumbi wa Nkurumah unawakilisha wasomi wa taaluma mbali mbali pale Mlimani, na Nyoka anawakilisha taaluma ya udaktari
ReplyDeleteMuulize Sheikh Yahya Husein ndo anajua maana zake hizo.
ReplyDeleteAlishawahi kuelezea kwenye vipindi vyake Star TV maana ya michoro/picha mbalimbali zilizopo kwenye noti za nchi mbali mbali duniani.
Elimu ya uganga. Hivyo inawakilisha wataalamu wetu wa chuo ch Muhimbili
ReplyDeleteAnawakilisha 'AFYA'
ReplyDeleteina represent kuwa nchi yetu na maskin wa kutupwa kaka michu
ReplyDeleteili peas iwe na nguvu inahitaji ushetani ndio maana pound ina wadada wawili wasionekana miguu wale ni majini na hii inaongezea nguvu. hii ni nyoioka na ni alama ya kijini inaongeza thamani ya pesa. ndio maana unaweza kuona hela zina kama alama a nyota hiyo pia ni alama ya kijini kwa kifupi ili hela ziwe na thamani huwa zinakuwa na alama za kijini . N yule ni nyoka kama moja ya alama ya kijini. kwa maelezo zaidi muona sheik yahya. Hii kwa maana mujibu wa kidununia.
ReplyDeleteAnawakilisha ushirikina wa watanzania. Kila sehemu uchawi tu makazini hata katika siasa uchawi uchawi uchawi tu na imani za kishirikina.
ReplyDeleteWote mmekosa,
ReplyDeleteinawakilisha tabia za viongozi wa bongo. Mambo ya kinyokanyoka tuuu.
huyu nyoka yuko karibu sehemu nyingi hata ulaya, amerika na sehemu nyingine kuna sehemu wameweka alama ya nyoka, sasa wewe unayesema tanzania uchawi nadhani ufanye utafiti ndipo useme kuliko kuandika vitu visivyo na uhakika.
ReplyDeletebro michu ngoja nikasake vitabu vinasemaje then nitatoa jibu. ila shekhe yahya aliwahi kuongea na kusema kwamba ni alama za majini.sasa kama ni alama za viumbe kama hao swali linakuja tena, je inafanya nini kwenye jero hiyo.
NOPE
kama watu wanafahamu baadhi ya alama za Free Mason ambazo ziko katika fedha zetu na taasisi mbalimbali zilizosimikwa na UN anaweza kujua habari za nyoka huyo kwenye fedha yetu, si nyoka chunguza utaona alama za piramidi, pembe tano katika baadhi ya fedha, utaona macho ya aina fulani yenye nyotanyota hivi, zote hizo ni alama ziko kwenye majengo, kwenye dollar, hata jengo la ikulu ya marekani lina baadhi ya hizo nilizo taja, zote ni alama za free mason. unaweza pia kuzikuta katika taasisi nyingi za UN.
ReplyDeleteni kwa vile tulio wengi hatujui ila tunatawaliwa na hawa free mason wao ndio wanashikilia World Bank IMF na UN, hakuna raisi anayetawala bila kupata baraka za hawa watu maana ndio wanaoshikili fedha ya ulimwengu, kuna mambo mengi yaliyofichika tusiyoyajua ila wadau wanaochunguza mambo ya ndani ya utawala wanafahamu ulimwengu unavyokwenda. Mambo mengine ni ya giza zaidi ndio maana wengine wanazungumzia yale ambayo shekhe Yahya amesema ni kwa sababu yaliyo mengi yanagusa ushetani zaidi maana kama mnajua hao free mason ni devil worshipers pia.
Michuzi na wadau wako tafuteni mambo haya kwenye mtandao mtapata yaliyo mengi, ila hapa ninapoishi last three weeks walionesha pia documentary ya Marekani inayozungumzia juu ya Free Mason, alama zao, maisha yao na imani kwa ujumla. Nawasilisha.
BWANA MICHUZI, ASANTE SANA KWA KUWEKA HIYO OJA HAPO JUU KWA HALI HALISI NINAONA KUWA WATU WENGI HAWAJUE MAANA YAKE HATA MIMI, KWA KUWA WEWE NDIO MPIGA PICHA AU MTU HAMBAYE UPO KWENYE MAMBO YA HABARI NILIONA KUWA NI VIZURI UTUPO UKWELI AU KAMA UNA UKWELI , FANYA JUU CHINI UOGEA NA WATU WA WIZARA YA FEDHA KAMA WAZIRI NA MAKATIBU WAKE NDIO WANAWEZAKUTUPA MAJIBU YAKE NA KAMA NA WAO NDIO KAMA SII NI VIZURI WAWAJIBIKE KWA SABABU NI KITU CHA HAJABU MTU KAMA WEWE KUWEKA HOJA KAMA HII BILA KUTAFUTA UKWELI WAKE...
ReplyDeleteNINAOGEJEA UKWELI , ASANTE
PIA NINAOMBA UWEKE PICHA CHA KULE MOSHI MAANA NIPO BRAZIL 20 YEARS NA PIA KUPA HONGERA KWA HII BLOG...:))))
Kaka Michuzi,samahani mimi nina ishu nyingne tofauti na mjadala huo hapo juu,nauliza hv;KWA NINI MAJENGO MENGI YANATOTUMIA LIFTI[ELEVATOR]HUWA UKISOMA NO KUANZIA 1 MPK 12 THEN NO 13 IMERUKWA INAFUATA 14 NI KWA NIN?naomba wadau wanisaidie kunipa jibu.
ReplyDeleteThis is quite interesting discussion. I tend to agree with those ones that associated the symbol with biblical holy words from old testament. It is interesting that the symbol was there for many years, but none was bothered to ask what it represents. The use of the symbol seems to be based on bible, the holy book. This shows how Tanzanians are dictated by religions with knowing that. Does anyone also know how the calendar that is widely used in the world got developed?
ReplyDeletehuyo anony aliyeuliza kwa nini kwenye elevetor wameruka no 13 hii ni kwa wamarekani wanaamini kuwa no13 ni bad luck ndo maana elevator zote za USA hukuti no 13 i hope umenipata
ReplyDeleteanony 12:25 sidhani kama una uhakika kwamba ni Americans ndio wana imani kuwa number 13 ni unluck number, nadhani hii imani ipo hata hapa kwetu bongo. Nenda PPF tower utakuta hakuna floor number 13.hii inadhihirisha kuwa hata jamii yetu tumeanza kuamini hili. Nyoka kwenye hela yetu ya Tanzania (jero) inaweza ikahusishwa katika hisia mbili tofauti. ya kwanza ni katika imani ya Kikristo na pili ni katika imani ya Freemasons ambayo alama hiyo inaitwa SERPENT. Katika imani ya Freemason inamaanisha utawala wa ulimwengu, inahusishwa hasa na nguvu za ushetani katika kuitawala dunia. sasa sijui viongozi wetu husika (Raisi, waziri wa fedha, gavana) wanatumaanishia nini kuwepo kwa nyoka na pyramids kwenye noti zetu.
ReplyDeleteNyoka = afya (masuala ya kiafya)
ReplyDeleteNyoka means huwezi kufanya kazi serikalini kama wewe sio nyoka (Usalama wa Taifa). Just kidding..
ReplyDeleteKuhusu namba 13...tazama hata ktk hotels, hakuna Room no. 13-- ila utakuta room no. 1215 ikimaanisha Room No, 15 iliyopo ktk ghorofa ya 12..Kwa hiyo hutakuta room number inayoanzia 13..unless iwe ni ya ghorofa ya 131 na kuendelea