wadau, kuuliza si ujinga. hivi huyu nyoka juu ya hili jero anawakilisha nini?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2007

    Kaka

    Mimi nafikiri, kwa vile walikuwa wanaenzi chuo Kikuu, cha Dar es salaam kwenye Jero,Huyo nyoka anawakilisha tiba, ambacho ni uwakilishi wa chuo kikuu kishiriki cha Muhimbili. Chunguza letter head za Muhimbili utagundua kuwa kuna nyoka. Wenyewe wanamwita nyoka wa utabibu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2007

    huyo nyoka anawakilisha rushwa, hilo jengo hapo ni benki kuu(hela). huwezi kuingia ndani yajengo(kupata hela) bila kumfurahisha nyoka(kutoa/kula rushwa)
    hiyo ndo bongo

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2007

    That's a Caduceeus, and has often used through out the centuries to represent health. In the states and other nations they use two snakes instead.

    The symbol's origins are thought to date to as early as 2600 BC in Mesopotamia, and there are several references to a caduceus-like symbol in the Bible, namely in Numbers 21:4­9, and 2 Kings 18:4. During the Exodus, Moses was instructed by God to fashion a pole upon which he was to position a serpent made of bronze; when looked upon, this Nehushtan, as it was called in Hebrew, would spare the lives of the Israelites stricken by venomous snake bites.

    The intent was that people would look upward and be reminded to pray to God, but eventually the meaning was forgotten and this symbol was apparently worshiped by the Hebrew people until the reign of Hezekiah as described in 2 Kings 18:4.Walter Burkert has two figures in his book which show a rod with two intertwined snakes winding around a central axis from Mesopotamia in 2200 BC, and a similar image from Crete in 700 BC.

    That's just a glimpse of the symbols history. Over the years it got adopted and transformed by different civilizations (e.g the Romans)

    For a more detailed history you can check out this link.

    http://www.crystalinks.com/caduceus.html

    ~Dave

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 21, 2007

    Ninajaribu kujibu swali la mwanakijiji mwenzetu alyeuliza maana ya alama ya nyoka iliyo katika noti. Sifahamu ni kwa nini serikali iliweka alama ila ninajua kuwa alama hiyo ina maana ya kiutabibu. Maana ya alama hiyo kiutabibu inatokana na simulizi lililomo katika Biblia kitabu cha Hesabu sura ya 21. Katika simulizi hilo inaonyeshwa kuwa baada ya Waisraeli kuondolewa utumwani Misri walimnung'unikia Mungu kuwa amewapeleka jangwani kusiko na chakula wala maji. Kwa sababu ya manung'uniko hayo, Mungu "aliwatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa" (Hes. 21:6). Baada ya kuona haya, watu wakamwendea Musa kiongozi wao na kusema, "Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu." Wakamwomba Musa awaombee kwa Mungu ili awasamehe na awaondolee wale nyoka. Musa alipomwomba Mungu kwa niaba ya watu wake, Mungu alimwambia Musa, "Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, na akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi" (Hes. 21:8-9).

    Kutokana na historia hii, mashirika mengi yanayohusika na mambo ya tiba yanatumia nembo hii ya nyoka aliyening'inizwa kwenye mti kama alama ya tiba.

    Kwa Wakristo, kifo cha Yesu msalabani kinabeba ishara ya nyoka aliyening'inizwa mtini. Ndiyo maana upo mkazo kuwa Yesu ni tiba ya magonjwa yote, ikiwa ni pamoja na gonjwa la dhambi. Mtu akimtazama yetu atapona, naam, ataishi.

    Sina hakika kama maana niliyoieleza hapa ndiyo maana iliyokusudiwa na walioiweka picha ya nyoka aliyening'inizwa kwenye mti katika noti. Inawezekana wana maana hiyo hiyo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 21, 2007

    Bro Michuzi

    Hy pengine ni alama ya afya!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 21, 2007

    anawakilisha madawa ya asili tuliyojaaliwa na mola

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 21, 2007

    Inawakilisha chuo kikuu upande wa Muhimbil.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 21, 2007

    Michuzi, hiyo noti upande huo umewekwa rasmi kwa ajili ya wanataaluma wa nchi yetu. Ukumbi wa Nkurumah unawakilisha wasomi wa taaluma mbali mbali pale Mlimani, na Nyoka anawakilisha taaluma ya udaktari

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 21, 2007

    Muulize Sheikh Yahya Husein ndo anajua maana zake hizo.
    Alishawahi kuelezea kwenye vipindi vyake Star TV maana ya michoro/picha mbalimbali zilizopo kwenye noti za nchi mbali mbali duniani.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 21, 2007

    Elimu ya uganga. Hivyo inawakilisha wataalamu wetu wa chuo ch Muhimbili

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 21, 2007

    Anawakilisha 'AFYA'

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 21, 2007

    ina represent kuwa nchi yetu na maskin wa kutupwa kaka michu

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 21, 2007

    ili peas iwe na nguvu inahitaji ushetani ndio maana pound ina wadada wawili wasionekana miguu wale ni majini na hii inaongezea nguvu. hii ni nyoioka na ni alama ya kijini inaongeza thamani ya pesa. ndio maana unaweza kuona hela zina kama alama a nyota hiyo pia ni alama ya kijini kwa kifupi ili hela ziwe na thamani huwa zinakuwa na alama za kijini . N yule ni nyoka kama moja ya alama ya kijini. kwa maelezo zaidi muona sheik yahya. Hii kwa maana mujibu wa kidununia.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 21, 2007

    Anawakilisha ushirikina wa watanzania. Kila sehemu uchawi tu makazini hata katika siasa uchawi uchawi uchawi tu na imani za kishirikina.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 21, 2007

    Wote mmekosa,
    inawakilisha tabia za viongozi wa bongo. Mambo ya kinyokanyoka tuuu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 21, 2007

    huyu nyoka yuko karibu sehemu nyingi hata ulaya, amerika na sehemu nyingine kuna sehemu wameweka alama ya nyoka, sasa wewe unayesema tanzania uchawi nadhani ufanye utafiti ndipo useme kuliko kuandika vitu visivyo na uhakika.

    bro michu ngoja nikasake vitabu vinasemaje then nitatoa jibu. ila shekhe yahya aliwahi kuongea na kusema kwamba ni alama za majini.sasa kama ni alama za viumbe kama hao swali linakuja tena, je inafanya nini kwenye jero hiyo.
    NOPE

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 21, 2007

    kama watu wanafahamu baadhi ya alama za Free Mason ambazo ziko katika fedha zetu na taasisi mbalimbali zilizosimikwa na UN anaweza kujua habari za nyoka huyo kwenye fedha yetu, si nyoka chunguza utaona alama za piramidi, pembe tano katika baadhi ya fedha, utaona macho ya aina fulani yenye nyotanyota hivi, zote hizo ni alama ziko kwenye majengo, kwenye dollar, hata jengo la ikulu ya marekani lina baadhi ya hizo nilizo taja, zote ni alama za free mason. unaweza pia kuzikuta katika taasisi nyingi za UN.
    ni kwa vile tulio wengi hatujui ila tunatawaliwa na hawa free mason wao ndio wanashikilia World Bank IMF na UN, hakuna raisi anayetawala bila kupata baraka za hawa watu maana ndio wanaoshikili fedha ya ulimwengu, kuna mambo mengi yaliyofichika tusiyoyajua ila wadau wanaochunguza mambo ya ndani ya utawala wanafahamu ulimwengu unavyokwenda. Mambo mengine ni ya giza zaidi ndio maana wengine wanazungumzia yale ambayo shekhe Yahya amesema ni kwa sababu yaliyo mengi yanagusa ushetani zaidi maana kama mnajua hao free mason ni devil worshipers pia.
    Michuzi na wadau wako tafuteni mambo haya kwenye mtandao mtapata yaliyo mengi, ila hapa ninapoishi last three weeks walionesha pia documentary ya Marekani inayozungumzia juu ya Free Mason, alama zao, maisha yao na imani kwa ujumla. Nawasilisha.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 21, 2007

    BWANA MICHUZI, ASANTE SANA KWA KUWEKA HIYO OJA HAPO JUU KWA HALI HALISI NINAONA KUWA WATU WENGI HAWAJUE MAANA YAKE HATA MIMI, KWA KUWA WEWE NDIO MPIGA PICHA AU MTU HAMBAYE UPO KWENYE MAMBO YA HABARI NILIONA KUWA NI VIZURI UTUPO UKWELI AU KAMA UNA UKWELI , FANYA JUU CHINI UOGEA NA WATU WA WIZARA YA FEDHA KAMA WAZIRI NA MAKATIBU WAKE NDIO WANAWEZAKUTUPA MAJIBU YAKE NA KAMA NA WAO NDIO KAMA SII NI VIZURI WAWAJIBIKE KWA SABABU NI KITU CHA HAJABU MTU KAMA WEWE KUWEKA HOJA KAMA HII BILA KUTAFUTA UKWELI WAKE...
    NINAOGEJEA UKWELI , ASANTE
    PIA NINAOMBA UWEKE PICHA CHA KULE MOSHI MAANA NIPO BRAZIL 20 YEARS NA PIA KUPA HONGERA KWA HII BLOG...:))))

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 21, 2007

    Kaka Michuzi,samahani mimi nina ishu nyingne tofauti na mjadala huo hapo juu,nauliza hv;KWA NINI MAJENGO MENGI YANATOTUMIA LIFTI[ELEVATOR]HUWA UKISOMA NO KUANZIA 1 MPK 12 THEN NO 13 IMERUKWA INAFUATA 14 NI KWA NIN?naomba wadau wanisaidie kunipa jibu.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 21, 2007

    This is quite interesting discussion. I tend to agree with those ones that associated the symbol with biblical holy words from old testament. It is interesting that the symbol was there for many years, but none was bothered to ask what it represents. The use of the symbol seems to be based on bible, the holy book. This shows how Tanzanians are dictated by religions with knowing that. Does anyone also know how the calendar that is widely used in the world got developed?

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 22, 2007

    huyo anony aliyeuliza kwa nini kwenye elevetor wameruka no 13 hii ni kwa wamarekani wanaamini kuwa no13 ni bad luck ndo maana elevator zote za USA hukuti no 13 i hope umenipata

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 22, 2007

    anony 12:25 sidhani kama una uhakika kwamba ni Americans ndio wana imani kuwa number 13 ni unluck number, nadhani hii imani ipo hata hapa kwetu bongo. Nenda PPF tower utakuta hakuna floor number 13.hii inadhihirisha kuwa hata jamii yetu tumeanza kuamini hili. Nyoka kwenye hela yetu ya Tanzania (jero) inaweza ikahusishwa katika hisia mbili tofauti. ya kwanza ni katika imani ya Kikristo na pili ni katika imani ya Freemasons ambayo alama hiyo inaitwa SERPENT. Katika imani ya Freemason inamaanisha utawala wa ulimwengu, inahusishwa hasa na nguvu za ushetani katika kuitawala dunia. sasa sijui viongozi wetu husika (Raisi, waziri wa fedha, gavana) wanatumaanishia nini kuwepo kwa nyoka na pyramids kwenye noti zetu.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 22, 2007

    Nyoka = afya (masuala ya kiafya)

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 22, 2007

    Nyoka means huwezi kufanya kazi serikalini kama wewe sio nyoka (Usalama wa Taifa). Just kidding..

    Kuhusu namba 13...tazama hata ktk hotels, hakuna Room no. 13-- ila utakuta room no. 1215 ikimaanisha Room No, 15 iliyopo ktk ghorofa ya 12..Kwa hiyo hutakuta room number inayoanzia 13..unless iwe ni ya ghorofa ya 131 na kuendelea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...