
wadau napenda kuomba radhi kwa kusema huko nyuma kwamba nancy sumary atakuwa ughaibuni na dada yake nakaaya. ukweli ni kwamba usiku kuamkia leo tulikuwa naye kwenye tuzo za kili music awards kama inavyoonekana hapa akiwa na klynn. aidha, tuzo hafla hiyo ambayo ilioneshwa hai na star tv kwa kushirikiana na tvt ilifana sana na sifa ziwaendee waandaaji pamoja na wadhamini ambao ni tbl kupitia kilimanjaro laga. chini pana mapendekezo mdau ambayo yameingia punde tu
Ninapenda kutoa mapendekezo yangu kuhusu utaratibu unaotumika hivi sasa katika utoaji wa tuzo ya heshima kwa wanamuziki mashuhuri wa TZ.
Kwa sasa hivi ni wanamuziki wawili to ndio waliopewa Tuzo ya heshima ya kudumu[MBARAKA MWINSHEHE MWARUKA na MARIJANI RAJABU MWANAMANYEMA] ambao kwa kweli sina ubishi na hilo kwani kila mpenda muziki wa asili ya TZ anakubaliana nalo kwa kura zote kabisa.
Lakini tatizo lililojitokeza ni kwa waandaaji wa TUZO hizi kuwasahau wanamuziki ambao walikuwa wakishindana kwa karibu sang na MAGWIJI hawa kwa kuwapa changamoto za hall ya juu na kuwafanya wasilale usiku wala mchana wakitafuta TUNGO za kushindana nao jambo lililopelekea kukua kwa muziki wa TZ na vipaji vyao kwa ujumla.
Mfano ni nani asiyejua jinsi tungo za HEMEDI MANETI ULAYA zilivyokuwa zikimlaza macho "JABALI LA MUZIKI LA TANZANIA?Nyimbo kama MATATA NDANI YA NYUMBA,NILIRUKA UKUTA,SALIMA,MARY MARIA,WIFI ZANGU MNANINYANYASA N.K. zilivyokuwa vikitingisha nchini na nje ya nchi. Aidha,ni mpenzi gain wa muziki asiyejua jinsi JUMA KILAZA alivyokuwa akimlaza macho "SOLOIST NASHIONALI" kwa tungo zake murua kwa kujibizana na hatimaye viwango vya muziki wa TZ kukua kwa kwenda mbele.
Vile vile,ni nani asiyejua mchango wa SALUM ABDALLAH katika maendeleo ya muziki wa TZ.Nawaomba waandaaji wa TUZO hizi kuwafikiria wanamuziki SALUM ABDALLAH, JUMA KILAZA na HEMEDI MANETI ULAYA kuwapa TUZO YA HESHIMA YA KUDUMU pia.
NAWATAKIA KILA LA HERI KATIKA SHUGHULI HII. - JOHN P. JAMBELE
misupu kwa kupenda wanawake bana, nambari moja.
ReplyDeleteNaomba tafadhali full pose picha ya nancy na klynn kwenye tuzo la kili
ReplyDeletehaloooooo jamani nauliza huyu nancy nywele za pembeni kapeleka wapi?Bongo hamna mawigi jamani????Aibu hii miss mzima kinyonyoke
ReplyDeleteSaw the show on TVT - that was just plain toooooo looooooong! I had to do a George Bush very often - switch to other channels (usually when George Bush comes on the screen)
ReplyDeleteunaji keep busy full time kipara lakini MVIII HIZO KWENYE KIPARA.lakini bado una pretend young.haya bwana retiring age hiyoo.
ReplyDeletewatoto wamependeza bwana big up bro michu nakuaminia wanaosema wapenda watoto wacha waseme kwa kuwa wao hawana bahati ya kukutana na hao ma misss. Ila yote tisa kumi nawazimia wote hao itabidi nimtafute mmoja wao kaka michu. Nancy anamacho ya mahaba sana na klyn mguu mzuri
ReplyDeletedada zangu nawashauri msiwe mnaweka manywele ya bandia mara kwa mara mnaona mwenzenu nancy nywele zote zimemnyonyoka
ReplyDelete